2017-11-14 15:53:00

Maskitiko ya Papa kwa waathirika wa tetemeko ardhi huko Iran na Iraq


Baba Mtakatifu ameonesha masikitiko makubwa kwa waathirika wa tetemeko la ardhi lilitokea jumapili kati ya nchi ya Iran na Iraq. Katika Telegram mbili zilizoelekezwa katika nchi mbili na kutiwa saini na Kardinali Pietro Paroli , Katibu wa Vatican, Baba Mtakatifu anaonesha huzuni kubwa kutokana na hali halisi  ya tetemeko iliyowakumba watu hao , anaonesha uwepo wake karibu kwa wote walioathirika. Kwa njia hiyo anasali na kuwakabidhi kwa Mwenyezi Mungu wa Huruma na kuwatakia baraka za kitume kwa wote ambao wako katika harakati za kuokoa. 

Takwimu za waathirika hadi sasa wamesema ni watu 454 waliokufa na watu zaidi ya 7000 ni majeruhi. Ni Tetemeko lililokuwa na nguvu katika mji ya Panjwin Iraq na Sulaimaniya karibu na Iran. Pamoja na hayo tetemeko limesikika hata katia Bara la Asia ya Kati.

Hali ni mbaya hadi sasa hasa katika miji ya milimani ya Sarpol-e Zahab mahali ambapo imeharibika na hata njia za kuweza kuwafikia watu wa wanaoishi huko. Amayasema hayo Balozi wa kitume wa Vatican Askofu Mkuu Leo Boccard aliye katika nchi ya Teharan na kutoa wito kwa watu wenye mapenzi mema kutoa msaada wa damu kwa ajili ya  kuwasaidia watu wengi waliojerihiwa  pamoja na kwa kwamba hospitali ya Sarpol-e Zahab karibu imeaharibika sana, lakini watu wengi bado wanahitaji msaada.

Sr Angela Rwezaula 
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.