Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Baba Mtakatifu Francisko \ Hotuba

Kalenda ya Ziara ya Kitume ya Papa nchini Cile na Peru imetolewa!

Ziara ya Kitume ya Baba Mtakatifu nchini Peru na Cile yapamba moto - RV

14/11/2017 16:27

Imetolewa rasmi kalenda ya Ziara ya Kitume ya Baba Mtakatifu Francisko ya kuelekea nchini Cile na Peru kuanzia tarehe 15 -18 Januari  nchini Cile  na tangu 18 -22 Januari 2018 nchini Peru. Nchi mbili za Amerika ya Kisini  zikiwa zinaunganishwa na lugha moja  lakini historia tofauti, ni nchi zinazowakilishwa na utajiri mkubwa wa kitasaufi na ubinadamu. 

Katika ujumbe wa Video uliotumwa Agosti mwaka huu kwa watu wa Peru, Baba Mtakatifu alikuwa akieleza kuwa siyo shahuku tu  bali hata nia ya kwenda katika nchi ili kukutan na watu wenye utajiri wa rasilimali nyingi. Hata hivyo akiongeza katika ujumbe wake , rasilimali nzuri sana waliyo nayo ni ule wa watakatifu nchi ya peru kwa maana watakatifu ni wengi katika Bara la Amerika ya Kusini.

Mwezi Februari mwaka huu wakati  Maaskofu a Baraza la Cile walikuwa kwenye matembezi ya kitume mjini Vatican, wakiwakilishwa na Kardnilai Ricardo Ezzetti Andrello ambaye ni Askofu Mkuu wa Santiago , katika mahojiano na waandishi wa habari mara baada ya kukutana na Baba Mtakatifu, alielezea juu ya mazungumzo yao na Baba Mtaktifu kuwa waliongelea juu ya furaha na mateso ,kwa mfano furaha ni ile yak ulna Kanisa lao katika nchi wanayo ibada kuu ya wawatu, ambayo ni nguvu ya kushangaza. Kwa nji ahiyo ratiba ya Baba Mtakatifu inaelekeza kuwa atawasili Santiago ya Cile tarehe 15 Januari jioni na kukutana na wafuatao: Viongozi, jamii ya umma na wanadiplomasia. Pamoja na hayo inatarajiwa matembezi binafsi ya Rais, na kufuatia Misa takatifu  katika uwanja wa  Mkubwa wa O’Higgins.

Mchana atatemblea Kituo Gereza la wafungwa wa kike wa Santiago, mapadre , watawa wote kike na kiume, waseminarisi katika Kanisa Kuu: Mkutano wa Maaskofu , Kutembelea Madhabahu ya Mtakatifu Alberto Hurtado na pia kukutana na kwa faragha na mapadre wa Shrika la Yesu (Wajesuit).
Siku itakayofuata, 17 Januari 2018, Baba Mtakatifu ataondoka huko Temuco kwa ajili ya Misa katika Uwanja wa ndege wa Maquehue na atakuwa na chakula cha mchana na baadhi ya wakazi wa  Aracaunia katika nyumba ya Mama wa Msalaba Mtakatifu (Madre de la Santa Cruz). Aturudi tena Santiago mahali ambapo mchana atakutana na Vijana katika Madhabahu ya Maipu, baadaye atatembelea Chuo cha Kipapa Katoliki nchini Cile.

Tarehe 18 Januari 2018 ataadhimisha misa katika Uwanja mkubwa wa Lobito ya Iquique , na kupata chakula cha mchana katika nyumba ya mafungo ya Madhabau ya Mama Yetu wa Lourdes (Nuestra Señora de Lourdes) inayotunzwa na Mapadre wa Shirika la  Waoblati.

Jioni ya saa 11 hivi Baba Mtaktifu ataondoka mjini Lima nchini Peru.  Katika hatua ya pili ya ziara ya baba Mtakatifu mara baada ya makaribisho na salam kwa viongozi wa nchi , atakutana na watu wa Amazon wa Mkoa wa Coliseo katika jimbo la Mama wa Mungu na watu wa Taasisi ya Jorge Basadre.Pia anatazamia kukutana na mfalme Hogar na kufanya mkutano wa faragha na Wajesuiti wa Kanisa la Mtakatifu Pedro.

Jumamosi 20 Januari 2018 Ataadhimihsa misa katika fukwe ya  Huanchaco; kuzunguka na gari katika mitaa itawayo “Buenos Aires” na baadaye watakutana na mapadre, watawa wote, waseminari  wa Kanisa katika  nchi ya Peru Kaskazini, itafuatia misa kwa heshima ya Bikira (Maria Virgen de la Puerta in Plaza de Armas).

Akitoka huko Lima siku inayofuata Baba Mtakatifu atashiriki masifu ya mchana na watawa  wa ndani katika Madhabahu ya Mama yetu wa miujiza. Asubuhi atasali mbele ya masalia ya watakatifu wa Peru katika Kanisa Kuu. Misa na Sala ya Malaika wa Bwana katika eneo la Uwanja wa ndege wa Las Palmas. Saa kumi na mbili na nusu jioni watafanya afla ya kumwaga tayari kuanza safasi ya kurudi Roma.

 Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 

14/11/2017 16:27