Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Baba Mtakatifu Francisko \ Hotuba

Jumapili 19 Novemba 2017 ni Siku ya Maskini Duniani !

Jumapili 19 Novemba 2017 ni Siku ya Masikini duniani mahali ambapo Baba Mtakatifu atashiriki meza ya Chakula Katika Ukumbi wa Mwenye heri Paulo VI Vatican - RV

14/11/2017 15:14

Tarehe 19 Novemba 2017 inaadhimishwa Siku ya Maskini duniani. Siku iliyopendekezwa na Baba Mtakatifu Francisko wakati wa kuhitimisha Jubilei ya Mwaka wa Huruma, ili jumuiya nzima ya kikristo iweze kujikita katika kuwafungulia mikono yao maskini, wadhaifu  na  wenye kukanyagwa hadhi yao ya kiutu.

Baraza la Kipapa kwa ajili ya Uinjilishi wamendaa tuko moja linaloendana na Siku kwa zaidi ya watu 4,000 wenye shida na maskini ambao watakuwa wamesikindikizwa na watu mbalimbali kutoka vyama vya kujitolea vya  mkoa wa Lazio nchini Italia na hata katika majimbo mengine ya dunia kama vile  kutoka miji ya ufaransa (Paris, Lione, Nantes, Angers , Beauvais, ; Uholanzi (Warsaw, Kraków, Solsona, Malines-Bruxelles e Lussemburg) kufika katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro ili waweze kushiriki misa ya Baba Mtakatifu Francisko itakayo anza jumapili majira ya saa 4.00 asubuhi masaa ya Ulaya.

Baada ya misa, watu 1,500 wamaealikwa katika Ukumbi wa Mwenye heri Paulo VI ili kushiriki chakula cha sikuu pamoja na Baba Mtakatifu Francisko. Siku hiyo bandi ya muziki ya Kikosi cha Ulinzi Vatican wataongoza hata kwa nyimbo  na kikundi ha watoto kuanzia miaka 5 hadi 14. Watu wengine 2,500 watapelekwa katika seminaari na Taasisi za kipapa za Amerika ya Kaskazini, Taasisi ya Kitume ya Leoniano , Kituo cha Mtakatifu Petro, Kituo cha Caritas Roma, Jumuiya ya Mtakatifu Egidio. Seminari Kuu ya Kipapa ya Roma, na Taasisi ya Kipapa ya Regina Apostolorum ili nao washiriki meza ya chakula cha sikukuu.

Maskini hawa watahudumiwa na mashemasi 49 kutoka katika majimbo ya Roma na watu wa kujitolea 159 kutoka katika maparokia ya majimbo tofauti. 
Baraza la Kipapa kwa ajili ya kuhamasisha uinjilishaji mpya wanatoa taarifa kuwa waliwashirikisha tangu mwaka 2016 mashirika ya kujitolea ambapo Ikiwemo Caritas Jumuiya ya mtakatifu Egidio, Chama kutoka katika kisiwa cha Malta, Nuovi Orienti, Mtakatifu Yohana wa XXIII, chama cha ndugu 2016,na vyama vingine vingi vinavyojihusisha kuwasaidia watu wenye matatizo na maskini ili kuweza kujaribu kuwakusanya watu hao wafanye sikukuu hiyo.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 

14/11/2017 15:14