Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Vatican \ Hotuba

Kard.Turkson:Maendeleo yawezekana kwa kuondoa silaha kwa ujumla!

Kardinali Turkson, yapo matokeo mabaya ya uharibifu wa sura ya mwanadamu kutokana na silaha za kinyuklia - AP

13/11/2017 16:25

Mtazamo wa dunia isiyo kuwa na silaha za kinyuklia na kusitishwa kwake kwa ujumla  ndiyo mada ya hati ya pamoja ya Mkutano wa Kimataifa  juu ya kusitishwa kwa silaha za kinyuklia, ulioandaliwa na Baraza la Kipapa kwa ajili ya Huduma ya Maendeleo ya Binadamu. Tukio hilo limefanyika tarehe 10 -11 Novemba 2017  kwa kuudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa dini , kisiasa,wenye Tuzo ya Nobel, wawakilishi wa jamii ya umma na mashirika ya kimataifa. 

Mkutano huo ulifungwa kwa hotuba na Kardinali Peter Turkson Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya Huduma ya Maendeleo ya Binadamu ambaye alisoma hitimisho la mkutano huo, ukiwa imejizatiti katika kila aina ya takafakari na malengo endelevu ya shughuli za kusitisha silaha za kinyuklia, maendeleo na amani.  Msisitizo wa hati hiyo kwa hakika unaunganishwa kati ya kusitisha kwa ujumla silaha za kinyuklia na maendeleo kamili. Kwa njia hiyo wito huo unachukua fursa ya  kukumbusha wito wa Baba Mtakatifu Francisko mara nyingi katika hotuba zake na hata katika Mkutano huo,akisisitiza kuwa, kila kitu kinaunganishwa kwa pamoja katika dunia hii. Tafakari kubwa ni kutoa kipaumbele zaidi cha kushutuma vikali wale wote wanatumia silaha za kinyuklia kwasababu ya kumiliki nyezo za uaharibifu  mkubwa wa maisha ya mwanadamu.

Aidha anakumbuka matokeo hasi  yaliyojitokeza katika baadhi ya nchi mbalimblia kutokana na kumiliki au kutumia silaha hizi za kinyuklia. Hati hii pia inaendelea  kufafanua wito wa Baba Mtakatifu  kuwa, kuzuia nyuklia haitoshi tu kuitikia mgogoro na changamoto za ulimwengu huu, pia udanganyifu wa kinyuklia hauwezi kuzuia au kukabiliana na vitisho vingi kama vile vya amani na usalama, ugaidi, migogoro isiyo ya kawaida, matatizo ya mazingira, na umasikini.

Kuzuia nyuklia siyo kujenga amani ya kudumu tu, bali ni katika kuzuia  silaha za uharibifu wa mkubwa, hasa silaha za nyuklia, ambazo  hazijengi chochote zaidi ya hisia ya uwongo wa usalama hata  kuunda utamaduni wa kutishiwa kwa pamoja katika mfumo wa kimataifa. Pamoja na hayo hati  inashutumu matumizi kwa kupoteza gharama nyingi za rasilimali zinazohitajika  kushughulikia sababu msingi za migogoro  na kukuza maendeleo na amani katika jamii ya watu duniani.

Jitihada za kusitisha silaha ni haja ya dharuraya haraka na mchakato wa muda mrefu , kwa maana kila kitu katika dunia kimeshikamana kwa mtazamo wa ekolojia kwa ujumla kama inavyoonesha Wosia wa Baba Mtakatifu Francisko wa Laudato Si. Kwa lengo hilo mazungumzo ni muhimu ambayo lazima yawe jumuishi kwa mataifa husika yanayotumia nguvu za kunyiklia, na yale yasiyo na nyuklia, yakihusisha jamii, mashirika ya kimataifa , serikali na jamuia za kidini kwa namna ya pekee Kanisa Katoliki ambalo linajizatiti katika kukuza mazungumzo haya kwa ngazi zote.

Hatimaye, katika hati ya mwisho ya Mkutano inatoa wito na kuwaalika nchi zote ambao hadi sasa  hawajasaini Mkataba wa kuzuia Silaha za Nyuklia ili wafanye hivyo na kuthibitishwa kwa Mkataba wa Kuzuia Silaha za Nyuklia. Kwa njia hiyo hati inatoa mwongozi ambao siyokuwalilisha majadilisnno bali zaidi ni kutoa mwanzo wa mazungumzo  na hatua endelevu.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio vatican

 

13/11/2017 16:25