2017-11-11 16:41:00

Papa amekutana na viongozi wa Jukwaa ya Sekretarieti ya Visiwa vya Pacific


Ninawashukuru  ninyi viongozi wa Kisiwa cha Pacific  (Leader del Pacific Islands Forum) katika Jukwaa la Sekreatarieti ya Kanda ambao katika uwepo wanu unaonesha utofauti wa hali halisi za Kanda ya Austraria utajiri na uzuri wa utamaduni na asili. Ni maneno ya Baba Mtakatifu aliyo anza nayo kuwakaribisha Viongozi wa  Jukwaa la Sekretarieti ya  Visiwa cha Pacific wanatoka  katika Bara la Australia, Visiwa vya Cook, Shirikisho la Visiwa vidogo vyote vya Asia , na Visiwa la Kaskazini vya Kifaransa, Kiribati, Nauru, New Zeland , Papua Guinea, Jamhuri ya Visiwa vya Marshall, Samora na Vanuatu  tarehe 11 Novemba 2017 mjini Vatican.

Viongozi hawa wamekuwa Roma siku zilizopita katika Mkutano wa juu kuhusu matatizo ya nchi zao hasa za Bahari ya Hindi na Pacific,  ambapo  Jumamosi tarehe 11 Novemba wameshiriki pia  Meza ya mduara katika Ofisi ya FAO mjini Roma ili kujadili juu ya usalama wa vyakula kikanda, lishe, mabadiliko ya hali ya hewa, upunguzaji wa majanga ya asili  na utekelezaji wake. Viongozi pia wataendelea na safari yao ili kuweza kushiriki Mkutano huko Bonn Ujermani  unaoendelea  wa Umoja wa Mataifa  COP23 juu ya hali ya Hewa.

Akiendelea na hotuba yake anasema, kwa bahati mbaya katika kanda yao kwa sasa inaishi kipindi cha wasi wasi mkubwa kwa kwa watu wote, kwa namna ya pekee watu wanaoishi  ndani yake, kwa maana ndiyo waathiriwa na matukio hali ya hewa mara kwa mara kwa kina. Pamoja na hayo pia anafikiria matukio mengine makubwa ya matatizo ya kuongezeka kwa maji kwa ngazi ya juu, pia hata mmomomyoko unaoendelea kuongezeka katika visiwa vingi muhimu duniani. Pamoja na hayo amekumbuka hata maswali yaliyulizwa miaka 30 iliyopita na maaskofu nchini Ufilipini kwamba “ni nani aliyebadilisha mshangao wa dunia ya bahari kuwa makaburi yaliyovuliwa maisha na rangi? “

Ni sababu nyingi zilizosababisha uharibufu wa mazingira hayo kwa bahati mbaya na mengi, na ndiyo pia yakasababisha hata ulemavu wa kibinadamu  ambao  pia unaunganishwa na aina nyingi za unyonyaji wa mali za asili na kibinadamu chini ya kina cha bahari. Tunapoongea juu ya ongezeko la maji bahari, ambayo hasa yanawakumba watu wanaoish fukweni, watu maskini ambao wanalazimika kuhama, ni lazima kufikiria pia matatizo ya ongezeko la joto ulimwenguni , ambao kwa sasa umekuwa mkubwa na unajadiliwa nna wengi nje ya mijadala ya kimataifa. Aidha Anakumbusha  kuwa wiki hii  unaendelea  Mkutano Cop23 wa kimataifa wa mabadiliko hali ya hewa mjini Bonn, Ujerumani kujadili jinsi ya kutekeleza makubaliano yaliyofikiwa Paris, yanayolenga kuzileta nchi pamoja kupunguza viwango vya joto duniani. Anasema ni nchi ambayao isiyokuwa na mipaka, kama vile walivyo ieleza wana hana wa Kituo cha Kazi katika Obiti alio zungumza nao hivi karibuni.

Pamoja na hayo wao wanatoka mbali sana na Roma kwa upeo wa Dunia isiyokuwa na mipaka, maana ardhi inaondoa umbali kijiograia,lakini ndiyo inawataka kuwa na  ulazima wa kuchukua hatua za madhuburi za dhamiiri ya dunia nzima, hasa kwa kushirikiana na mshikamano wa kimataifa, kuwa na mikakati shirikishi ambayo inapinga utofauti  mbele ya matatizo makubwa kama ya mabadiliko ya hali ya hewa, uangalizi wa mabahari makubwa , ambayo yanaunganisha na maisha ya kibinadamu ndani ya jamii ya leo inayoishi.

Halikadhalika anasema, haijalishi umbali kijografia na maeneo, bali hata muda ambao unaondolewa kwa utambuzi ya kwamba ndani ya ulimwengu kila kitu kimeunganishwa pamoja: kwa mfano imepita miaka 30 tangu wito wa Maaskofu wa Ufilipini walipotoa kauli ya utetezi wa mazingira katika hali halisi ya mabahari , lakini hadi leo hii hakuna kilichobadilika, badala yake ni kuona idadi kubwa ya matatizo ambayo tunaweza kuitwa kuwa ni matokeo ya usimamizi mbaya  wa mali asili za majini, uchafuzi wa kupindukia wa bahari kwa njia ya plasitiki na kadha wa kadha.

Baba Mtakatifu anaongeza swali je ni ulimwengu upi tunao tamani kuonesha kwa kizazi kitakachofuata baada ya sisi, watoto ambao wanazidi kukua? Swali hilo halihusu mazingira tu bali  tunapotafakri juu ya ulimwengu tunao tamani ni lazima kutazama mwalekeo kwa ujumla kwa maana ya thamani yake .

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.