2017-11-10 09:02:00

Kuanzaia 2018 Sigara hazitauzwa kwa wafanyakazi na wastaafu Mjini Vatican


Katika kutoa jibu la swali kwa wanahabari, kuhusiana na uamuzi wa Baba Mtakatifu kukatisha kuuza sigara kwa wafanyakazi  na wastaafu wa Vatican, Msemaji Mkuu wa Vatican Bwana Grek Burke amethibitisha hilo kuwa Baba Mtakatifu ameamua kuwa Vatican itaacha kuuza sigara kwa wafanyakazi  na wastafu wa Vatican kuanzia 2018. Na sababu yake Bwana Burke anasema ni rahisi:

Hawali ya yote Vatican haiwezi kuchangia zoezi la huaribifu wa afya za watu!  Akifafanua zaidi anasema, kwa mujibu wa Shirika la Afya duniani, kila mwaka  moshi wa sigara unaua watu zaidi ya milioni saba ulimwenguni. Hivyo basi, ingawa sigara huuzwa kwa wafanyakazi wa Vatican na wastaafu kwa bei nafuu kulingana na chanzo cha mapato cha Vatican  lakini  hakuna faida inayoweza kuwa halali ikiwa inahatarisha maisha ya watu, anathibirisha!


Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kisahili ya Radio Vatican
 
 

 








All the contents on this site are copyrighted ©.