Tarehe 8 Novemba 2017 Baba Mtakatifu Francisko amekuta na Kardinali Angelo Amato, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya Kuwatangaza Wenye heri na Watakatifu. Katika Mkutano wao, amekubali maombi ya kutambuliwa kuwatangazwa wenyeheri na watakatifu wafuatao:
Mtumishi wa Mungu Giovanni Brenner, Padre wa jimbo. Alizaliwa tarehe 27 Desemba 1931 huko Szombathely (Ungheria) na kuwawa kwa ajili ya kutetea imani yake tarehe 15 Desemba 1957.
Mfadini Mtumishi wa Mungu Leonella Sgorbati, mwanashirika la Kimisionari wa Konsolata. Alizaliwa 9 Desemba 1940 huko Rezzanello ya Gazzola (Italia) na kuwawa kwa ajili ya kutetea imani yake tarehe 17 Septemba 2006 huko Mogadishu (Somalia). Utambuzi wa uadilifu wa mwenyeheri Bernardo di Baden, Marchese di Baden; aliyezaliwa kati ya mwa mwaka 1428 na 1429 huko Hohenbaden (Ujerumani) na kifo chake tarehe 15 Julai 1458 huko Moncalieri (Italia).
Utambuzi wa uadilifu wa mtumishi wa Mungu Papa Paolo I (Albino Luciani). Alizaliwa tarehe 17 Oktoba 1912 huko Agordo (Italia) na kifo chake tarehe 28 Septemba 1978 katika nyumba ya Kitume Vatican.
Utambuzi wa uadilifu wa Mtumishi wa Mungu Gregorio Fioravanti, Padre wa Shirika la Ndugu Wadogo wa Mtakatifu Francisko na Mwanzilishi wa Shirika la Watawa wa Kimisionari wa Moyo Mtakatifu. Alizaliwa huko Grotte ya Castro (Italia) tarehe 24 Aprili 1822 na kifo chake huko Gemona (Italia) tarehe 23 Januari 1894;
Utambuzi wa uadilifu wa Mtumishi wa Mungu Tommaso Morales Pérez, Padre wa Shirika la Wajesuit na Mwanzilishi wa Taasisi katoliki za Kilei za Cruzados na Cruzadas de Santa María; Alizaliwa huko Macuto (Venezuela) tarehe 30 Oktoba 1908 na kifo chake tarehe 1° Oktoba 1994 huko Alcalá de Henares (Hispania);
Utambuzi wa uadilifu wa Mtumishi wa Mungu Marcellino da Capradosso, Msekulari wa ndugu wadogo wakapuchini . Alizaliwa tarehe 22 Septemba 1873 huko Villa Sambuco ya Castel ya Lama (Italia) na kifo chake tarehe 26 Februari 1909 huko Fermo (Italia);
Utambuzi wa uadilifu wa Mtumishi wa Mungu Teresa Fardella mjane wa Blasi, Mwanzilishi wa Shirika la watawa wa Kike wa Wana wa Maria Mtakatifu, aliyezaliwa huko New York (Marekani) tarehe 24 Mei 1867 na kifo chake tarehe 26 Agosti 1957 huko Trapani (Italia).
Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican
All the contents on this site are copyrighted ©. |