2017-11-09 16:05:00

Papa:Jifunze Vema Mafundisho Jamii ya Kanisa ili kukabiliana na changamoto!


Baba Mtakatifu amekutana na kuzungumza na Jumuiya Taasisi ya Kipapa ya Ukrane ya Mtakatifu Yosephat mjini Roma. Katika Hotuba yake, amemshukuru Kardinali Leonardi Sandri Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya Makanisa ya mMshariki, Monsinyo Vasil Katibu wake na Gombera wa Taasisi hiyo kwa maneno ya utangulizi wa Hotuba yao.

 Anasema makutano yao yanakuja katika tukio la kumbukumbu ya  miaka 85 ya kuanzishwa kwa Taasisi hiyo kwa utashi wa Papa Pio XI. Yeye alianzisha shughuli hiyo  kwa namna ha pekee na udhati kama Kharifa wa Mtume Petro kuonesha ukarimu na undugu kwa waamini wa Makanisa yanayotokea kwenye maeneo ya matatizo na mateso, ili kwa namna ya pekee wajisikie hapa Roma kama watoto wanaopendwa na kuishi nyumbani,  kukua wakijiandaa  katika utume wa kimisionari wa kishemasi na kikuhani.

Katika miaka hiyo ya Utwala wa Papa Pio XI alilazimika kukabiliana na changamoto za nyakati , lakini daima aliendela kutoa sauti yake kutetea imani, huru wa Kanisa na hadhi ya kila binadamu. Yeye aliweza kupinga vikali hata kwa maeno na nyarka , itikadi kali za kupinha Mungu na zile za ukosefu wa maisha ya kibandanu ambazo zilizasababisha umwagaji damu katika karni ya 20.Na kwa njia hiyo akweka mwanga wa hali halisi na kuonesha Kanisa njia mwalimu ya Injili  hasa kuijikia katuka matendo ya kutafuta haki za kijamii,kulingana na maisha ya watu na hata kwa ajili ya Taifa.

Kutokana na ushuhuda wa Papa  Pio XI, Baba Mtakatifu Francisko amewaomba wao kama makuhani wa siku zijazo, wajifunze vema Mafundisho Jamii ya Kanisa ili kuweza kukomaa katika kung’amua na kuthibiti hali halisi ya jamii ambayo watatakiwa  hudumia  katika siku za mbeleni.
Katika nyakati zetu Baba Mtakatifu anaendelea, duniani imejaa majeraha ya vita, vurugu na migogoro kwa namna ya pekee hata katika nchi yao ya Ukrane. Mahali ambapo wao wnatokea, na watatakiwa kurudi baada ya masomo yao Roma.  Baba Mtakatifu anasema, ni mahali ambapo watu wengi wanafanya uzoefu wa mateso ya kila aina na kusababisha waathirika  wengi.

Na kwa njia hiyo wao watatakiwa  kutafuta haki amani dhidi ya mambo ya kijamii kama vile ifisadi au sera za siasa zinazo zidi  kuifanya nchi iwe maskini kwa wale wanaolipa ni maskini zaidi. Wao pia wanaalikwa  kuwa mashuhuda katika hai katika hali halisi hiyo. Hivyo Baba Mtakatifu anaongeza kusema, Bwana wape ujasiri wote wanao jikita katika kuhakikisha kwamba jamii inakuwa yenye haki na mshikamano.

Zaidi kwa wasiminari na mapadre wote wa Kanisa Katoliki la Kigiriki huko Ukrane , anasema kuwa Changamoto hizi ninaweza kuonekana kuwa ni nje ya uwezo wao lakini wakumbuke daima maneno ya Matakatifu Yohane kuwa nawaandikia ninyi vijana kwasababu mmeshinda ulimwengu na Neno la Mungu libaki nanyi. » (1 Yh 2,13.14). Kulipenda na kutangaza Neno hilo, litawaimarisha na kugeuka kuwa wachungaji wema wa Jumuiya ambazo watapewa ili wawe ndiyo taa inayo angaza mioyo na nyumba zao. Baba Mtakatifu ameongeza, na hiyo ni kwa ajili ya wote wanaojiandaa hata katika ukuhani na kila aina ya utume kulingana na utamaduni wa Kanisa lao. Ili pia wao waweza kupenda na kuwafundisha wengine msingi wa mazungumzo ya kiekumene katika hali halisi ya nchi zao.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.