Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Vatican \ Hotuba

10-11 Nov. Vatican kutakuwa na Mkutano wa Kimataifa juu ya Silaha za Kinyuklia

Tarehe 10-11 Novemba, utafanyika Mkutano wa Kimataifa mjini Vatican kuhusu Ulimwengu usio kuwa na silaha za kinyuklia - EPA

09/11/2017 16:04

Tarehe 10-11  Novemba 2017 utafanyika  Mkutano wa Kimataifa wenye kauli mbiu  "Matarajio ya ulimwengu huru usiokua na silaha za nyuklia na silaha muhimu" mjini Vatican katika ukumbi wa Sinodi, uliyoandaliwa na Baraza la Kipapa kwa ajili ya huduma ya Maendeleo ya Binadamu.
Kardinali Peter K.Turkson,Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya huduma ya Maendeleo Binadamu wakati wa maandalizi ya Mkutano huo  amesema kuwa tukio linajibu vipaumbele vya Baba Mtakatifu katika Amani na matumizi ya viumbe kwa ajili ya maendeleo na ubora wa maisha kwa watu wote bila tofauti.

Hata hivyo Askofu Bruno Marie Duffé, Katibu Baraza la Kipapapa kwa ajili ya  huduma ya Maendeleo ya watu, katika mkutano wa kimataifa wa nishati ya atomiki huko Viena tarehe  12-18 Septemba 2016, alisisitiza umuhimu wa jukumu la maadili kwa mataifa na changamoto ya mkakati wa kawaida wa mazungumzo.

Huu ndio mkutano wa kwanza wa kimataifa wa silaha za nyuklia tangu kutiwa idhini ya Mkataba wa Kuzuia Silaha za Nyuklia, uliyosainiwa na nchi 122 katika jumuiya ya kimataifa ikiwa ni pamoja na Vatican huko New York mnamo tarehe 7 Julai 2017 baada ya miaka ya machungu na mazungumzo yenye uchovu, hatimaye  saini zikawekwa  katika mji huo huo tarehe 20 Septemba 2017.

Kwa hali hiyo, Mkutano huo utakua na ushiriki wa pamoja wa Tuzo ya Amani ya Nobel, Mkutano wa Umoja wa Mataifa na NATO, wawakilishi wa kidiplomasia wa nchi ikiwa ni pamoja na Russia, Marekani, Korea Kusini, Iran, pamoja na wataalam wa juu wa silaha na maonesho, mashirika ya kiraia ambayo yamekuwa yakishiriki kwa muda mrefu. Pia wawakilishi wa Makanisa ya Kiekumene na dini nyingine,walimu na wanafunzi kutoka Vyuo Vikuu vya Umoja wa Mataifa, Urusi na Umoja wa Ulaya.

Kwa namna ya pekee  pia utoaji wa ushuhuda wa Masako Wada, Katibu Mkuu Msaidizi wa Nihon Hidankyo, mmoja wa waathirika wa mwisho wa mabomu huko Hiroshima, ambaye atawakilisha waathirika wa silaha za kinyuklia na waathirika wa majaribio mengine ya silaha za kinyuklia.Kutoka Vatican itawakilishwa na Katibu Kardinali Pietro Parolin, na wakuu  Baraza la Kipapa kwa ajili ya hudma ya Maendeleo ya binadamu.

 Baba Mtakatifu Francisko atawapokea na kuzungumza nao katika Ukumbi wa Clementina mjini Vaticana tarehe 10 saa sita mchana masaa ya Ulaya.
Pamoja na Baraza la Kipapa kwa ajili ya Maendeleo ya Watu, kuandaaa wanashirikiana na Ubalozi wa Italia Vatican, Kituo cha Sayansi kwa ajili ya Amani (Cisp); Chuo Kikuu cha Pisa; Baraza la  Maaskofu wa Japani; Baraza la  Maaskofu Ujerumani; Chuo Kikuu cha Georgetown; Taasisi ya Kroc ya Mafunzo ya Amani ya Kimataifa ya Chuo Kikuu cha Keough cha Mambo ya Ulimwengu; Mazda Motor Ulaya GmbH; Chuo Kikuu cha Notre Dame, Ofisi ya Rais; Mpango wa kuangamiza nguvu za Nyuklia; Mikutano ya Pugwash juu ya Sayansi na Mambo ya Dunia; Soka Gakkai International na Umoja wa Wanasayansi wa Silaha (Uspid).

Frt Tito Kimario 

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 

09/11/2017 16:04