2017-11-08 16:07:00

Papa ametuma Telegram ya salam za Rambi rambi kwa Kanisa la kibatisti Texas


Baba Mtakatifu Francisko katika telegram iliyosainiwa na Katibu wa Vatican Pietro Parolin, na kuielekeza kwa Askofu Mkuu Gustavo García-Siller huko  Mtakatifu Antony Texas Marekani, anaonesha masikitiko na uchungu mkubwa  kwa ajili ya habari za mashambulzi ya Kanisa ambapo watu wamepoteza maisha yao na wengine  majeruhi katika Kanisa  la Kibatisti la Sutherland Springs.

Baba Mtakatifu anaomba salam zake za rambirambi ziwafikie wanafamilia wote wa waathirika na majeruhi na wanajumui la Kanisa hilo ikiwa ni pamoja na  jumuiya nzima ya Texas. Mwisho wa Telegram, Baba Mtakatifu anaomba sala kwa Mwenyezi Mungu aweze kuwatuliza wote wanao omboleza kwa ajili ya wapendwa wao. Mungu awajalie nguvu za kiroho na kushinda migogoro, chuki na ili izaliwe nguvu mpya ya kusamehe, kuwa na  matumaini na upendo katika maridhiano.

Ikumbukwe ilikuwa ni siku ya Jumapili tarehe 5 Novemba 2017  Devin Kally  wakati wa ibada ya Misa ya asubuhi ya waamini  alifyatua risasi kwa waamini wa Kanisa la Kibatisti la mjini  Sutherland Springs huko Texas.
Akizungumza mara moja baada ya tukio hilo  Mwenyekiti wa Baraza la Maskofu wa Marekani Kardinali Daniel DiNardo amesema ni tukio ambao ni la kutisha kwa jumuiya nzima.

Aidha Taarifa zinasadikika kuwa ni watu 26 ambao wameuawa kwa kupigwa risasi na mtu kwa kufyatua  risasi hovyo kwa waumini katika Kanisa wakati  wanasali na wengine 20 kujeruhiwa. Mshambuliaji, ambaye anadaiwa kuuawa baada ya kutekeleza mauaji hayo, aliingia kanisani na kuanza kuwafyatulia risasi watu mwendo wa saa tano unusu asubuhi za Marekani. Gavana Greg Abbott amethibitisha idadi ya waliofariki na kusema ndicho kisa kibaya zaidi cha mauaji ya kutekelezwa kwa kutumia bunduki katika historia ya texas. Ni majonzi na masikitiko mengi kwa wale walioathiriwa. 

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.