Tarehe 7 Novemba 2017 Baba Mtakatifu Francisko amekutana katika ofisi binafsi ya Ukumbi wa Mwenye heri Paulo VI Imam Mkuu wa Al- Azhar, Profesa Ahmad Muhammad Al-Tayyib na wajumbe wake.
Hii ni kwa mara ya tatu Baba Mtakatifu Francisko kukutana na Kiongozi wa Kiislam wa Suuni ili kujadiliana naye. Mara ya kwanza ili kuwa mnamo tarehe 23 Mei 2016 mjini Vatican, na mara ya pili mjini Cairo Misri tarehe 28 Aprili 201 , wakati Baba Mtakatifu aliposhiriki tukio la Jukwaa ya Amani huko Al Azhar akiwa katika ziara yake ya kitume nchini Misri.
Kwa upande wa wote wawili, tukio la kukutana limekuwa la muhimu hasa katika kujadiliana zaidi juu wa wajibu wao pamoja wa kujikita katika mchakato wa amani dhidi hali za kisasa zinazoendelea kuibuka za kiitikadi kali za kidini na ugaidi.
Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican
All the contents on this site are copyrighted ©. |