Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Kanisa Barani Afrika \ Maisha Ya Kanisa Afrika

Askofu Cornelius Korir wa Jimbo la Eldoret-Kenya ameaga dunia!

Askofu Cornelius Korir wa Jimbo la Eldoret nchini Kenya ameaga dunia tarehe 29 Oktoba na mazishi yake yatafanyika tarehe 11 Novemba 2017 - RV

08/11/2017 10:30

Maaskofu Katoliki nchini Kenya wanaomboleza kifo cha marehemu Askofu Cornelius Arap Korir kilichotokea  usiku wa  tarehe 29 Oktoba 2017 nyumbani kwake huko Eldoret. Akithibitisha kifo hicho cha ghafla katika jimbo la Eldoret, Mwenyekiti wa KCCB na Askofu wa Homabay Philip Anyolo amesema, Askofu Korir alitakiwa kupelekwa Nairobi kwa matibabu zaidi mnamo tarehe 30 Oktoba 2017. Lakini  siku aliyotakiwa kwenda, Padre alipokwenda kumwona hakuwa ameamka. Daktari aliitwa na kuthibitisha  kwamba askofu hakuwa tena hai. Kwa upande wao anasema, Kanisa limekumbwa na  huzuni sana.

Akizungumza na waandishi wa habari tarehe 30 Oktoba, 2017 huko Eldoret, Askofu Anyolo alitangaza kuwa Misa Takatifu itafanyika kila siku katika Kanisa la Eldoret kuanzia saa 1.00 mchana masaa ya Afrika ya Masahariki  kwa ajili ya marehemu  Askofu mpaka hapo  atakapopumzishwa katika nyumba yake ya milele. Mpaka alipofikwa na umauti, Askofu Korir alikuwa Mwenyekiti wa Tume Katoliki na Haki ya  na Amani ya  Baraza la Maaskofu Kenya (KCCB) na Askofu wa Eldoret.

Alijulikana sana kwa nafasi yake katika kutetea amani na kupinga ukiukwaji wa haki za kijamii na kwa sababu hiyo viongozi wa kidini kutoka jumuiya za madhehebu mengine chini ya mwavuli wa Kikundi cha Mazungumzo (DRG) ambapo alikuwa pia ni mwenyekiti.
Kikundi hiki kinajumuisha uongozi wa juu kutoka Mkutano wa Baraza la Maaskofu Katoliki wa Kesnya (KCCB), Halmashauri ya Taifa ya Makanisa nchini Kenya (NCCK), Baraza Kuu la Waislam wa Kenya (SUPKEM) na Baraza la Viongozi wa Kiislamu (NAMLEF), Baraza la Hindu Kenya (HCK), Shirikikisho la Kiinjili Kenya (EAK) na Shirika la Makanisa la Afrika (OAIC), Seventh Day Adventist (SDA) na Shia Ithna-Asheri.

Askofu Korir alizaliwa mnamo tarehe  6, Julai,1950. Alipata daraja la Upadre  mwaka 1982 na baadaye akachaguliwa kuwa Askofu Jimbo la  Eldoret mnamo tarehe 2 Aprili 1990. Askofu Korir alikuwa miongoni mwa viongozi wa Kanisa Kaskazini mwa Kenya ambaye amekuwa akionya viongozi wa kisiasa dhidi ya maneno ambayo yanaweza kuwagawa Wakenya kwa ukabila. Marehemu Askofu Korir atazikwa Jumamosi, tarehe 11 Novemba 201.
 Apumzike kwa amani.

 

08/11/2017 10:30