2017-11-03 09:33:00

Papa katika Makaburi ya Nettuno amesema,Vita ni uharibifu wetu sisi!


Misa ya marehemu wote kwa upande wa Baba Mtakatifu, imeadhimishwa saa 9.15 mchana masaa ya Ulaya katika Makaburi wa Waamerika, waliokufa kipindi cha Vita ya II ya Dunia, ambao wamelala katika Makaburi ya Nettuno Wilayani Roma.
Mara baada ya kuwasili kwa gari dogo, kabla ya kuanza ibada Takatifu, Baba Mtakatifu amesimama kidogo katika Makaburi, na kati ya hayo hata yale ambayo hawajulikani, mwamerika mmoja na myahudi. Mikononi mwake alikuwa na maua kumi ya mawaridi meupe ambayo aliweza kuweka moja baada ya nyingine makaburini akiwa anatembea taratibu. Mara baada ya tukio hilo amekaribishwa katika sakrestia na Askofu Marcello Semeraro wa Jimbo la Albano, Mkurugenzi wa Makaburi Melanie Resto na mameya wa Nettuno Angelo Casto, na Luciano Bruschini wa Anzio

Baba Mtakatifu katika mahubiri yake aliyotoa bila kuandika anaelezea sura makini na sauti hasa ile ya mateso mbele ya majanga ya migogoro, lakini baadaye anafakari juu ya matumaini ambayo mkristo anapaswa kuwa nayo, anasema, wote wamekusanyika pale kwa matumaini na kwamba wanaweza kurudia maneno ya Ayubu katika Somo la Kwanza , yasemayo mimi natambua kuwa mwokozi wangu ni hai ambaye nitamwona… Anaongeza,  Matumaini ni yale ya kukutana na Mungu na kukutana na wote, kama asemavyo Mtume Paulo katika somo la pili kwamba matumani hayakatishi tamaa.
Matumanini lakini mara nyingi yanazaliwa na kuweka mizizi yake katika majeraha ya binadamu, kwa maana kuna uchungu wa kibinadamu, na kipindi cha majeraha ya mateso ambayo yanatufanya tutazame juu angani. “Sisi tunaamini kuwa Bwana yu hai na yupo nasi, na kwa njia hiyo angoza,” basi tumwambie simama Bwana”.

Akiendelea na mahubiri hayo Baba Mtakatifu Francisko amerudia mara tatu akisema, kamwe visitokee vita, na majanga haya yasiyo faa. Kama alivyokuwa amesema hata Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto wa XVI. Ni bora kuwa na mategemeo bila kuwa na uharibifu wa vijana, mamilioni matumanini yaliyokatishwa maisha yao. Amerudia kwa kusisitiza kama mbiu ya maombi, “vita hivi visirudiwe ee Bwana”.
Sala ni muhimu leo hii katika dunia, mahali ambapo vita na wengine wanajiandaa kwa nguvu zote kwenda katika vita. Katika vita kila kitu kinapotea ameendelea Baba Mtakatifu akisimulia juu ya mzee moja mbele ya uhalibifu wa Hiroshima, alisema; watu wanafanya kila njia kufanya vita na mwisho wanajiharibu wao wenyewe. Kwa njia hiyo anaongeza, “vita hivi ni uhalibifu  wetu wenyewe.
 
Ni siku ya matumaini na hata machozi yasitiririke kwa siku hii. Kwa maneo hayo   amekumbuka wanawake wengi na mama wakati wa kipindi cha vita  Kuu ya pili ya dunia, walikuwa wakisubiri barua, lakini barua zilileta habari za vifo vya waume na watoto wao. Hayo ndiyo machozi ya binadamu ambayo yasisahaurike anasema Baba Mtakatifu. Anaongeza;  hiyo inatokana na kiburi cha binadamu ambao hawataki kujifunza somo na kujifanya kwamba hawana haja ya kujifunza.

Hata hivyo anasisitiza kusema, matunda ya vita ni kifo. Ni mara ngapi binadamu anafikiria kufanya vita akiamini kuwa ndiyo njia ya kupelekea ulimwangu mpya, katika kipindi cha demani, lakini baadaye anaishia katika kipindi cha vuli, ukatili, na ufalme wa hofu na vifo. Sala ya Baba Mtakatifu kwa namna ya pekee ni kwa ajili ya vijana wengi wanaokufa katika mapambano ya vita katika maeneo mbambali,wakiwemo hata watoto pia. Anaomba sala kwamba "Ee Bwana  utoe neema ya kulia".

Saa 10.30 Jioni Baba Mtakatifu alianza safari ya kurudi mjini Roma mara baada ya kuwasalimia kwa namna ya pekee wafanyakazi wote wa Makaburini  
Katika upeo wa kikristo , maana ya kifo ni ufunguzi wa matumaini, ni kwa neema ya Kristo kama inavyosomekana katika Katekismu ya Kanisa Katoliki. Kwa maana hiyo kifo cha mkristo kina maana yake , kwani hata Mtakatifu Paulo anasema kuishi kwangu ni Kristo na kufa ni faida(Fil 1,21).  Ni hakika maneno hayo kwasababu tunapokufa na yeye tutaishi hata na yeye(2Tm,211). Kwa maana hiyo kifo ni upeo wa faida kwasababu unatufikisha katika Muungano kamili na Kristo.

Hata upeo wa Kifo unaelezewa vema katika liturujia ya Kanisa , kwamba mbele ya waamini Bwana, maisha haya kutolewa , bali kubadililishwa. Katika Katekekismu ya Kanisa Katoliki bado inaeleza kuwa mwisho wa hija ya binadamu ni mwisho wa neema na huruma ambayo Mungu anaitoa katika maisha yake hapa duniani katika mtazamo wa kimungu kwa ajili ya kuchagua hatma yake.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 

 








All the contents on this site are copyrighted ©.