2017-11-01 15:05:00

1 Novemba ni Sikukuu ya Watakatifu wote: tambua viungo vya Heri ya Utakatifu!


“Katika Sikukuu Watakatifu wote ni sikukuu yetu pia na  hiyo siyo kwamba sisi ni wema, bali utakatifu wa Mungu unagusa maisha yetu. Watakatifu hawana mifano timilifu, lakini ni watu waliopitia kwa Mungu. Tunaweza kuwafananisha na vioo vya Kanisa vinavyo ruhusu mwanga wa rangi mbalimblai ingie ndani yake. Watakatifu ni ndugu kaka na dada ambao walipokea mwanga wa Mungu katika mioyo yao na kutoa mifano halisi wakiionesha katika dunia kulingana na uwezo wao (rangi). Lakini wote wamekuwa na maisha yaliyokuwa wazo na wamepambana ili kutoa mabakabaka na giza la dhambi, hivyo wakaruhusu kwa ukarimu na  mwanga wa Mungu uingie ndani ya maisha yao na  ndilo lengo la maisha yetu”

Ni Maneno ya Baba Mtakatifu Francisko aliyo anza nayo tarehe 1 Novemba 2017 wakati wa  sala ya Malaika wa Bwana kwa mahujaji wote waliokusanyika kusali naye Sala ya Malaika wa Bwana wakati Kanisa Katoliki linaadhimisha sikukuu ya Watakatifu Wote. Baba Mtakatifu anaendelea: “Injili ya leo inawaeleza watu wote kwamba Heri ninyi”… (Mt 5,3). Ni neno linalo anza kwa kuonesha kwamba, ni Injili ambayo ni Habari njema  kwasababu inaonesha njia ya furaha. Aliye na Yesu ni mwenye heri pia anayo furaha. Furaha haitokani na mambo mengi  au mtu yoyote; furaha ya kweli inatokana kwa Bwana na kuishi kwa upendo naye. Baba Mtakatifu ameulizwa swali mahujaji wote iwapo wanakubaliana naye au hapana !...

Na kama wanakubaliana japokuwa ni wachache, lakini ni lazima kwenda mbele kwa kuamini hilo, na pia ametoa orodha ya  mchanganyo wa viungo vinavyoleta furaha ya kweli ya  maisha  kwamba ni Heri. Katika kuorodhesha amesema, ni wale wenye upole, wanyenyekevu wanao mwekea Mungu  nafasi, wanao omboleza kwa ajili ya wengine, wanaolinda usafi wa moyo, wakarimu, wanaopambana kwa ajili ya haki, wenye huruma  wasio kuwa na chuki hata kama wanateseka, wanaojibu vyema dhidi ya mabaya.

Huo ndiyo mchanganyo wa viungo vya Heri anasema Baba Mtakatifu. Haitoshi kuwa na  ishara za kiajabu, au ushujaa  bali ni kuwa  mtu anayeishi na majaribu na ugumu wa kila siku. Ndiyo watakatifu hao  ambao wanavuta hewa ya ubaya uliopo katika ulimwengu huu lakini katika safari hiyo  hawapotezi kamwe upeo wa Yesu, ambao umeelekezwa katika heri hizo, kwa maana anaongeza, ndiyo ramani ya maisha ya kikristo.
Leo hii ni sikukuu ya wale waliofikia kikomo ambacho kimeelekezwa na ramani hiyo. Baba Mtakatifu anathibitisha kwamba,  lakini siyo watakatifu waliopo katika kalenda tu, pia hata kwa ndugu na kaka wengi walioko katika milango ya jirani, ambao labda tumekutana nao, tunawafahamu. Hii ni sikukuu ya familia anasema,  ya watu wengi rahisi  waliofichika lakini kiukweli wanamsaidia Mungu ili ulimwengu huu uendelee mbele. Anasisitiza, “Leo hii wapo wengi sana”!  pamoja na hayo ameongeza kusema tuwashukru kaka na dada wasio julikana ambao wanamsaidia Mungu ili ulimwengu uende mbele , wanaishi katikati yetu, tuwasalimie na kuwapigia makofi!.....

Akiendelea na mahubiri anasema, hawali ya yote,  heri ya kwanza ni masikini wa roho (Mt 5,3). Ni nini maana yake? Ni wale wasioishi umaarufu, au kutawaliwa na fedha, maana wanatambuwa kuwa mtu anayejirundikia mali kwa ajili yake mwenyewe hana  utajiri mbele ya Mungu. (Lk 12,21). Aidha wanaamini kwamba Bwana ndiye tunu msingi wa maisha, na upendo wa ndugu ndiyo chemi chemi ya faida hiyo. Baba Mtakatifu ametoa mfano :mara nyingi tunalalamika juu ya jambo linalokosa na  kuhangaika iwapo hatupati kile ambacho tunataka, lakini lazima kukumbuka kwamba, mambo hayo hayapo katika heri  bali yupo  Bwana na upendo wake, ni Yeye peke yake wa kupendwa na kuishi heri hizo, Baba Mtakatifu amesisitiza.

Na mwisho wa mahubiri  amesema kuwa, anapenda kuongeza  heri ambayo haipatikani katika Injili lakini inapitikana katika mwisho wa Biblia isemayo mwisho wa maisha. Hiyo inapatikana katika kitabu cha ufunuo (Uf 14,13): Heri watu ambao tangu sasa wanakufa wakiwa wameungana na Bwana. Naye Roho anasema, Naam ! Watapumzika kutoka taabu zao maana matunda ya jasho lao yatawafuata. Kutokana na kipengele hicho Baba Mtakatifu amesem tarehe 2 Novemba tunaalikwa kuwasindikiza kwa maombi  kwa namna ya pekee marehemu wote  ili waweze kufurahi na Bwana. Tuwakumbukee kwa shukrani ndugu zetu wapendwa na kusali kwa ajili yao. Amemalizia Baba Mtakatifu! akisema Mama wa Mungu, Malkia wa Watakatifu na Mlango wa Mbingu atuombee katika safari ya Utakatifu na kwa ajili ya ndugu zetu waliotutangula katika Mbingu Takatifu.

Sr Amgela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.