2017-10-30 09:06:00

Papa:Upendo wa kweli na Mungu unatokana na kumpenda jirani yako


Yesu aliishi maisha yake yote akihubiri na kutenda kile ambacho kinahesabiwa na muhimu yaani upendo. Ni maneno ya Baba Mtakatifu Francisko aliyonena kwa nguvu kabla ya sala ya Malaika wa Bwana kwa mahujaji wote waliokusanyika katika viwanja vya Mtakatifu Petro Jumapili 29 Oktoba 2017. Baba Mtakatifu ameonesha kuwa, upendo unatoa msukumo na kutoa maisha,ni safari ya imani kwa maana bila upendo maisha na imani vinabaki tasa.
 
Akitakari Injili ya Siku kutoka (Mt 22,34-4), maahali ambapo Mwinjili Matayo anakumbusha kuwa, wafarisayo wanatoa swali la mtego, juu ya amri ipi iliyo kubwa. Katika kuelezea, Baba Mtakatifu anasimamia zaidi kufafanua juu ya upendo kati ya Mungu na binadamu. Amekumbusha jibu lake Yesu:mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, kwa roho yako yote na akili yako na mpende jirani yako kama wewe binafsi.
 
Kwa njia hiyo Yesu anataka utambuzi ya kwamba bila upendo wa Mungu na jirani, hakuna uaminifu wa kweli wa agano la Bwana. Baba Mtakatifu anaongeza, wewe unaweza kufanya mambo mema mengi, hata kutimiza sheria, lakini kama hauna upendo mambo hayo hayasadii kitu.
Akitaja kitabu cha somo la Kutoka, mara nyingine anasema, huwezi kuwa na agano na Bwana wakati wewe unawatesa wale walio chini yako: hawa ni wajane, yatima, wageni, wahamiaji yaani watu wote wapweke wasiokuwa na mlinzi. Baba Mtakatifu anasisitiza kwa nguvu zote kuwa, sisi sote tumeumbwa kwa ajili ya kupenda na kupendwa kama Injili inavyojieleza yenyewe ambayo inajibu shuhuku halisi ya moyo.
 
Mungu ni upendo anaendelea Baba Mtakatifu, ametuumba tuwe sehemu yake ya maisha, kwa ajili ya kupendwa na Yeye na kwa ajili ya kumpenda, na ile kwa ajili yake tuwapende wengine. Hiyo ndiyo ndoto ya Mungu kwa Binadamu. Ni ndoto inayowezekana kwa njia ya neema yake tu, kwasababu sisi tunahitaji kuipokea ndani mwetu ili tuwe na uwezo wa kupenda, upendo utokao kwa Mungu mwenyewe. Hiyo kwa dhati inatolewa na Yesu katika Ekaristi Takatifu ambayo ipo kwa ajili ya kuelezea upendo wake mkubwa alio utoa yeye binafsi kwa Baba yake kwa ajili ya ukombozi wetu.
 
Mara baada ya Sala ya Malaika wa Bwana, amewasalimia wahujaji wote walio kusanyika katika uwanja wa Mtakatifu Petro ambapo Baba Mtakatifu amekumbuka kutangazwa kwa mwenye heri mpya Giovanni Schiavo tarehe 28 Oktoba huko Caxias de Sul nchini Brazil. Alizaliwa mwanzoni wa mwaka 1900 nchini Italia, lakini akatumwa kwenda kufanya umisionari  akiwa ni padre nchini Brazil na kujikita zaidi katika huduma ya watu wa Mungu na kwa  kuwafundisha watawa wa kike na kiume. Mfano wake,  Baba Mtakatifu ameongeza, utusaidie kuishi kikamilifu katika kumfuasa Kristo na Injili. Aidha amewasalimia wanajumuiya ya Togo wanao ishi nchini Italia na wale wa nchi ya Venezuela, akiwakabidhi wote chini ya Mama Maria wa matumaini hasa katika nchi zao.
 
Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.