2017-10-30 15:08:00

Kard.Filoni anasema upendo wa Yesu unajipanua katika kukaribisha


Jumapili 29 Oktoba 2017, Kardinali  Ferdinando Filoni  Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya Uinjilishaji wa watu , ambaye yuko Uganda katika hitimisho la maadhimisho ya Jubilei ya Miaka 50 ya Jimbo Kuu la Kampala, ameadhimisha Misa Takatifu katika Madhabahu ya Mashahidi wa Uganda kuhitimisha Sikukuu hiyo yenye kauli mbiu “Fanya Kumbukumbu , furahi na kubadilika”. Katika mahubiri yake ya  Injili ya Jumapili ya 30 ya Kipinchi cha Mwaka wa kawaida , ametafakari maeno ya  Yesu akithibitisha amri ya kwaza iliyo kuu ya kumpenda Mungu kwa moyo wote sawa na kupenda jirani kama nafsi yako.

Kardinali akifafanua, amesema ni kama wakristo ni lazima kujibu maneno ya Yesu kwa kusikiliza kilio cha masikini, wagonjwa, wanaobaguliwa, wahamiaji , wakimbizi, waathirika wa migogoro ya kivita na wale walio katika matatizo ya ukosefu wa hadhi yao. Haitoshi tu kuzungumzia juu ya matukio hayo bali inahitajika kukabiliana na mahitaji yao.  Ni lazima kauwasaidia watu wengi ambao wamekimbilia Kampala kutoka nchi nzima ya Uganda kutafuta maisha bora, japokuwa wamebaki pembeni mwa jamii na kubaguliwa. Pamoja na hayo amewaeleza wasisahahu hata maelfu ya wakimbizi kutoka nchi ya Sudan ya Kisini ambao wamefika Uganda kutafuta mahali pa usalama kwa ajili ya maisha yao dhidi ya vurugu nchini mwao. Amesisitiza zaidi kwamba wasiwaache peke yake kwa hali yoyote waliyo nayo hata ya kidini.

Upendo ambao Yesu anataka, hauishii kati ya mahusiano ya ndugu tu, bali mahusiano yanayojipanua na kuendelea katika jumuiya hadi kugeuka upendo wa kijamii na hata kisiasa katika kutafuta mema kwa ajili ya wote. Baada ya kuwashukuru kwa furaha ya kukua kwa Jumuiya hiyo ya kanisa kwa miaka 50 ametoa wito wa kuanza jitihada mpya ya kuinjilishaji  kwa mtazamo wa Mtaguso wa II wa Vatican na juu ya maelekezo ya  Waraka wa Kitume wa Kanisa Barani Afrika,(”Ecclesia In africa”)  wa Mtakatifu Yohane Paulo II.

Katika Waraka wake wa kitume wa Mtakatifu Yohane Paulo II, kwa Kanisa Barani Afrika,( “Ecclesia in Africa”) anapenda kuihamasisha Familia ya Mungu Barani Afrika kuhakikisha kwamba, inatumia vyema njia za mawasiliano ya kijamii kama nyenzo ya kueneza Habari Njema ya wokovu. Njia za mawasiliano zinawaunganisha watu wengi, kiasi cha kuufanya ulimwengu kuwa kama kijiji. Familia ya Mungu Barani Afrika inakumbushwa kwamba, Kanisa linatumwa kutangaza na kushuhudia Injili inayookoa na kuponya. Pamoja na Waraka wa Africae Munus wa  Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto wa XVI. Huu ni Waraka kwa Kitume baada ya Sinodi anao waandikia Maaskofu, Makleri, watu walio weka wakfu, waamini Walei juu ya Kanisa Barani Afrika katika kuhudumia upatanisho, haki na amani, wenye kauli mbiu  “NINYI NI CHUMVI YA DUNIA ... NINYI NI NURU YA ULIMWENGU” (Mt 5:13-14)

Kwa kumalizia anasema, jitihada za uinjilishaji inapaswa zijikite katika Injili kwa kwa kina, siyo tu katika mioyo ya mtu binafsi , bali hata katika jamii nzima ili mahusiano ya kijamii kiuchumi daima iongozwe na roho ya kikristo na kujenga utamaduni wa upendo, mapatano, haki na amani.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.