2017-10-30 10:31:00

Kard Parolin awatia Moyo watu wa Norcia baada ya mwaka 1 wa Tetemeko la ardhi


Baba Mtakatifu anawatia moyo ili kuanza safari kwa upya, na wasiache kamwe kuelemewa na kushindwa na matatizo, badala yake watazame mbele kwa matumaini ya wakati ujao. Ni maneno ya Kardinali Pietro Parolin Katibu wa Vatican akiwakilisha Baba Mtakatifu katika moyo wa Norcia nchini Italia wakati wa maadhimisho ya misa mbele ya Kanisa Kuu la Mtakatifu Benedikto Jumapili 29 Oktoba 2017 . Ni Misa katika kukumbukumbu ya mwaka mmoja baada ya tetemeko la ardhi nchini Italia, lililotokea kati ya tarehe 26 na 30 Oktoba 2016 na kusababisha kuyumba maisha ya watu wengi wa Mikoa ya Umbria, Marche na Lazio.
 
Kardinali Parolin anaendelea kusema, Baba Mtakatifu anawataka wawe na imani kwa Mungu na Mama yake Maria ili kupata nguvu ya lazima kupeleka mbele kwa ujasiri ukarabati na ujenzi mpya wa maeneo yao. Tetemeko la ardhi lililoharibu hata Kanisa Kuu la Mtakatifu Benedikto, Kardinali anafafanua, bado ni jaribio katika uwezo wa kibinadamu ili kuweza kuamka tena na kutumaini, kwa kutazama mbele na juu ya Mbingu kwa nguvu zote. Aidha katika mtazamo mpya, hata kwa akili, ubunifu na kujikita zaidi katika huduma ya pamoja katika ujenzi wa nyumba, Kanisa na hata maadili ya binadamu kama vile jumuiya na kurudia furaha ya kuishi maisha mapya.
 
Akitafakati juu ya masomo ya Siku ya Jumapili kuhusiana na upendo wa jirani na Mungu, Kardinali anasema, matendo na kuabudu Bwana, ndiyo kiini cha uwajibikaji wa kuhudumia binadamu, maana Mungu anaonekana kwa jirani anayetolewa ushuhuda wa upendo. Na hiyo ni dhahiri kwamba, siyo rahisi kupenda ki ukweli jirani iwapo hauna upendo wa Bwana, vilevile  hata huna upendo wa kweli iwapo humpendi jirani.
Ni Mungu anayetoa amani ndani ya roho ili kutambua upendo wake Yeye japokuwa anaongeza, upendo wa jirani unakabiliwa na hatari kubwa hasa ile ya kubaki na upendo wa kijujuu tu. Bila upendo kutoka kwa Mungu siyo rahisi kuwa na mapatano dhidi ya adui, iwapo uhusiano na Mungu siyo thabiti, tunaishia kutokuwa na uvumilivu kwa sababu ya vizingiti vyetu na hata majeraha yanayotokana na vizingiti hivyo.
 
Akitumia hata maneno ya Mtakatifu Yakobo yasemayo: ina maana gani kusema kuwa unayo imani iwapo huna matendo mema? anaongeza mtume Yakobo, imani bila matendo imekufa. (Yk 2, 14-17)”.
Mtakatifu Yohane Krizostom anasema, kama unataka kuabudu mwili wa Yesu, usiruhusu mwili huo ukawa kitu cha kudharauliwa katika mwili wa maskini, wasio kuwa na nguo ya kujifunika. Kwa kufuata mifano hiyo Kardinali anaongezea juu ya ya Injili ambapo mafalisayo wanataka kumweka Yesu katika matatizo kwa njia ya maswali yao juu ya amri kuu. Lakini jibu la Bwana anaema, linawaweka kwenye kioo cha kuangaza kila dhamiri ambayo inathibitisha kuamini Mungu peke yake, na kuwaalika wakiri imani yao kwa njia ya huruma, ukarimu kwa jirani hasa wenye kuhitaji na kwa ajili ya wote.
 
Kwa mujibu wa Kardinali Parolini, anathibitisha kusema lakini kwa njia hii ya ukarimu ndiyo imekwenda sambamba na matendo katika majanga ya asili yaliyojitokeza maeneo ya Norcia na sehehemu zote za Kati. Mara baada ya tetemeko hili kuendelea  kupamba moto, lakini na ukarimu ulipamba moto, kila moja alijotoa muda wake, nguvu zake, fedha na hata watu wengi kujitahidi katika kuwasaidia wengi wenye kuhitaji msaada.
 
Ametumia fursa hiyo kuwashukuru vikosi vya ulinzi, zima moto, na mashirika mbalimbali ya serikali kwa mshikamano mkubwa walioonesha katika Kanisa la Spoleto-Norcia, ikiwa pia msaada kutoka Vatican na baadhi ya majimbo na Mabaraza ya Maaskofu, hata ukarimu wa parokia, vyama vya kitume, na mashirika ya dini kwa kuwasaidia Caritas ya Jimbo na Taifa
 
Pamoja na hayo Kardinali Pietro Parolin anakumbuka hata jitihada kubwa za Taasisi za Ulaya kwa usimamizi na uwekezaji   wa kazi ya kukarabati kwa upya Kanisa Kuu la Mtakatifu Benedikto, wakiwa na utambuzi wa nafasi yake iliyonayo Kanisa hili ambayo haiwezekani kubadilishwa kwa ajili ya Ulaya, Ukristo na katika utamaduni ambao Kanisa Kuu hilo limeweza kuutoa kwa karne nyingi.
 
Kwa kumalizia , Kardinali Pietro Parolin ametoa pia wito kwa Taasisi zote za Kanisa na binafsi, kushirikiana kwa pamoja na watu wenye mapenzi mema ili kuweza kufikia malengo ya ukarabati huo , kwa njia ya mkakati uliooneshwa tangu hawali ya tetemeko la ardhi. Ni muhimu kuongeza nguvu ili kuweza kuzuia kuhama kwa watu katika maeneo yao kutokana na kurudia tetemeko amesema.
 
Misa imaeadhimishwa saa tano asubuhi masaa ya Ulaya katika Uwanja wa Mtakatifu Benedikto wa Norcia.  Kabla ya Misa ametoa salam kwa niaba ya watu wote Askofu Mkuu Renato Boccardo wa Jimbo Kuu la Spoleto na ambaye ameomba Kardinali Pietro Parolin afikishe salam na shukrani zao za kina kwa Baba Mtakatifu kwa ukaribu wake na kuwatiwa moyo katika miezi hii kwa wazalendo hao.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.