2017-10-26 17:50:00

Papa:Mshikamano na ushirikiano wa Kikristo ndiyo viwe ushuhuda daima


Alhamisi 26 Oktoba 2017, Baba Mtakatifu Francisko amekutana na kuzungumza na Wawakilishi wa Kanisa la Scoltland mjini Vatican, ambapo amewakaribisha kwa furaha na shukrani kwa kwa hotuba iliyotolewa,  kwamba uwepo wao ni kumpa fursa ya kutoa salam zake za dhati kwa watu wote wa Kanisa la Scotland.

Mkutano wao unajitokeza katika ukaribu wa kuadhimisha miaka 500 ya mageuzi ambapo yeye binafsi aliungana nao katika kumbukumbu huko Lund Sweden mwaka mmoja uliopita. Shukrani kwa Bwana kwa zawadi ya kufikia mwaka  huu katika kuishi kama ndugu na siyo tena kuwa tofauti na migogoro iliyojitokeza kwa miaka  mingi. Kwa uwezo wa neema ya Mungu katika safari ya kiekumene, anasema Baba Mtakatifu imewesha kujikita kwa kina kuwa na utambuzi , matumaini na mshikamano wa dhati kati yetu.

Ukaribu huo wa kusafisha kumbukumbu ni moja ya matunda msingi katika safari hiyo. Hata kama zamani kumekuwapo na mitafaruko lakini leo hii upo utambuzi na hatimaye kuanza kuwa na upeo mpya na mtamzao wa Mungu kjuu etu.Sisi wote hawali ya yote ni watotowa mUngu tunaozaliwa katika Kristo kwa njia ya ubatizo ,ambao tunapata masumbuko na mateso, utofauti , makosa na matarajio ya mioyo kutokana na ubaguzi na mateso yaliyo jitokeza.
Aidha ametoa mfano wa Injili inayo elezea juu ya kuteswa ,kwamba ni lazima kuendelea na njia ya upendo wa unyenyekevu ambao unashinda migawanyiko na kuponya majeraha. Kwa kuwa tayari katika safari ya mazungumo ambayo imeanza , lakini inaweza kufikia utilifu wake kwa njia ya kuinjilishwa kwa maana ndiyo hali halisi ya kutangaza Mungu wa upendo (1 Yh 4,8).

Lakini katika nchi ya Scotland kwenye mji wa Edimburg , zaidi ya miaka mia moja iliyopita, wakristo wamisionari , walijulikana sana katika kufanya mapenzi ya Yesu asemavyo, uli ulimwengu upate kuamini (Yh 17,21). Wao walitambua ya kwamna kutangaza na utume ,haviamiki iwapo aviendani na umoja, yaani daima umoja wa dhati kama hapo hawali. Aidha Baba Mtakatifu amekumbuka kwa namna ya pekee wakristo wangi wenye majaribu , kwasababu ya kuteswa kwa ajili ya jina la Yesu , maana wanasadiki hadi kufia dini , ni wengi na wanabeba msalaba. Ushuhuda wao lakini unatoa nguvu ya kuendelea mbele kwa ujasiri hadi kufika mwisho.Kwa njia hiyo ni lazima wote kuendelea na mazungumzo, ushuhuda, huduma ya pamoja na shughuli ya kusali kwa ajili ya mmoja kamili.

Baba Mtakatifu  Francisko anamalizia akisema kuwa, anaomba ili safari kuelekea umoja unaoonekana , uweze kuendelea kila siku na kutoa matunda mengi katika siku zijazo, kama ilivyokuwa hawali. Kanisa Katoliki kwa namna ya pekee kupitia Baraza la Kipapa kwa ajili ya kuhamasisha umoja wa Kikristo, anaongeza, linajikita kwa miaka miaka mingi sasa likionesha matunda ya ushirikiano na Kanisa la Scotland, pamoja na Umoja wa Makanisa ulimwenguni , ambayo bado wanashahuku na kupenda  hiyo safari ya pamoja .Kwa njia ya uwepo wao wa safari ya Kiekumene, Baba Mtakatifu amewaombea nguvu ya Roho Mtakatifu kuwaimarisha na kuwapa nguvu wote katika  umoja wa Kristo Yesu.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.