Uhuru wa mtu unaharibika unapojikabidhi katika nguvu kiziwi cha dhamiri na hasa ya kutaka kupata mahitaji ya haraka na ubinafsi. Ni maneno ya Baba Mtakatifu Francisko katika hotuba yake kwa lugha ya kihispania kwa jumuiya Chuo Kikuu Katoliki cha Kireno, alipokutana nao asubuhi ya tarehe 26 Oktoba 2017 katika tukio la mwaka wa 50 wa kuanzishwa kwake.
Baba Mtakatifu ansisitiza hayo akikumbuka waraka wake wa “Laudato si “ Sifa kwa Bwana ya kwamba ni ujumbe wazi ambao uweze kuendelea kukua bila kuwa na zana ya kuuzuia. Hiyo ni kwasababu ya kuzingatia mafikiano ya kikundi ambacho kinakosa uamininfu na maadili ya thabiti , utamaduni, tasaufi ya kweli inayoweza kutoa kweli uthibiti na kutunza utawala wake binafsi.
Kwa njia hiyo Baba Mtakatifu ametoa swali muhimu ya kwamba je tunawasaidiaje wanafunzi wetu wasione shahada ya chuo kikuu kama vile ni pesa kubwa au ufahari mkubwa wa kijamii? Sio ulinganifu huo tu bali hata kujibu swali jingine ya kwamba, ni muhimu kuwa thabiti. Ukweli wa kuwa mkatoliki Baba Mtakatifu anaongeza ni kipengele kisichohukumu Chuo Kikuu. Kinyume chake, kinatoa thamani kubwa, kwa upande huo anakumbusha hasa hatua ya Waraka wa Kitume wa Mtakatifu Yohane Paulo wa II juu ya vyuo vikuu Katoliki.Waraka wake umeandikwa kuwa, msingi wa Chuo Kikuu ni jitihada za kutafuta ukweli kwa njia ya utafiti, kuhifadhi na mawasiliano ya ujuzi kwa manufaa ya jamii”.
Inaweza kuzingatiwa kuwa, mafundisho ya chuo kikuu hufanya hitimisho lake katika
imani anasema Baba Mtakatifu, Lakini mafundisho Katoliki, hayazungumzi kama mwakilishi
wa imani, lakini juu ya yote kama shahidi halali kwa sababu ya maadili. "
Hatimaye Baba Mtakatifu anakumbuka mwisho nini maana ya chuo kikuu Katoliki pia
na nini mana ya kuwa Mreno. Anasema, maswali ya watu wengi yanatufanya kutafakari
juu ya mapambano yao, ndoto na wasiwasi ya kwamba vyote hivyo vina thamani kubwa
ambayo hatuwezi kupuuza. Bwana alikuja ndani ya ulimwengu na kwa njia hiyo, hatuwezi
kupata uokovu nje ya ulimwengu wetu halisi.
Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican
All the contents on this site are copyrighted ©. |