Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Baba Mtakatifu Francisko \ Katekesi siku ya Jumatano

Papa:Katekesi ya mwisho kuhusu mada ya Matumaini ya Kikristo

Baba Mtakatifu Francisko baada ya kumaliza Katekesi yake Jumatano mjini Vatican tarehe 25 Oktoba 2017.

25/10/2017 16:51

Walipofika mahali paitwapo, “Fuvu la Kichwa,” ndipo wakamsulubisha Yesu pamoja na wale wahalifu wawili, mmoja upande wake wa kulia na mwingine upande wake wa kushoto. Vilevile maandishi haya yalikuwa yameandikwa na kuwekwa juu yake: “Huyu ndiye Mfalme wa Wayahudi.”  Mmoja wa wale wahalifu waliotundikwa msalabani, alimtukana akisema: “Je, si kweli kwamba wewe ndiwe Kristo? Basi, jiokoe mwenyewe, utuokoe na sisi pia.” 40 Lakini yule mhalifu mwingine akamkemea mwenzake akisema: “Wewe humwogopi Mungu hata kidogo? Wewe umepata adhabu hiyohiyo.  Wewe na mimi tunastahili, maana haya ni malipo ya yale tuliyotenda. Lakini mtu huyu hakufanya chochote kibaya.” Kisha akasema, “Ee Yesu! Unikumbuke wakati utakapoingia katika ufalme wako.”  Yesu akamwambia, “Nakwambia kwa hakika, leo utakuwa pamoja nami peponi.”

Wapendwa, hii ni katekesi ya mada ya mwisho kuhusu  matumaini ya Kikristo, ambayo imetusindikiza tangu mwanzo wa mwaka wa kiliturujia. Ninamaliza nikizungumzia  juu ya peponi kama mahali pa matumaini yetu. Peponi ni mojawapo ya neno la mwisho aliyotamka Yesu msalabani, aliyomgeukia mhalifu mwema.  Ni maneno ya Baba Mtakatifu Francisko aliyo anza nayo wakati wa Katekesi yake ya kila Jumatano mjini Vatican tarehe 25 Oktoba 2017. Baba Mtakatifu anasema, hebu tusimame kidogo na kuona tendo hilo hilo. Kutazama juu ya msalaba na Yesu peke yale. Kulia na kushoto wapo wahalifu wawili. Labda mbele ya misalaba ile mitatu huko Golgota, kuna  aliyepitia na kupumua kidogo akifikiria kwamba, atimaye tendo la haki limefanyika kwa ajili ya kifo cha wale watu!

Mbele ya Yesu lakini yupo  muungama, kwa maana anatambua makosa yake ya kustahili  adhabu kubwa. Na ndiyo huyo anayeitwa mhalifu  mwema kwani anamwambia hata mwenzake, ya kwamba wanastahili adhabu kutokana na matendo yakeo (Lk23,41). Baba Mtakatifu anaendelea kubainisha kuwa, njia ya msalaba wa huko Kalvario siku ya Ijumaa Takatifu Yesu alifika juu na  kuonesha nini maana ya kutwaa mwili, au mshikamano wake kwetu sisi na wadhambi. Ni kutilimiza kile kilichotabiliriwa na  Nabii juu ya mtumishi wa mwenyezi Mungu,  “kwa hiyo nitamweka katika cheo cha wakuu,  atagawa na nyara pamoja na wenye nguvu, kwa kuwa alijitolea mwenyewe kufa akajiachia kuwa kundi moja na wakosefu, alizibeba dhambi zake  kwa ajili ya watu wengi akawaombea msamaha hao wakosefu. (Is 53,12; na  Lk 22,37).

Baba Mtakatifu anasemam ni Kalvario ambapo Yesu anafanya mkutano wa mwisho na mdhambi, kwa ajili ya kumfungulia yeye milango ya ufalme wake. Neno Peponini lilipata fursa kwa mara ya kwanza katika  Injili anasema Baba Mataktifu. Yesu alimwahidi huyo mhalifu  ufalme wake, kwakuwa alipata ujasiri wa kumwelekeza maombi yake, kwa unyenyekevu, yeye hakuwa na lolota mbali na kumtegemea Yesu vilevile kutambua Yesu kuwa hana hatia tofauti na yeye. Baba Mtakatifu anaongeza kusema, ilitosha maneno ya kuungama kwa unyenyekevu , ambayo yaligusa kwa kina moyo wake Yesu.
Mhalifu mwema Baba Mtakatifu anasema, anatukumbusha hali yetu halisi mbele ya Mungu:kwa maana ya kwamba sisi ni watoto wake, Yesu anakuwa na uchungu kwa ajili yetu, yeye hana silaha mkononi mara tu tunapo mwendea na kumuonesha ule shahuku ya upendo wake. Aidha Baba Mtakatifu anasema katika vyumba vya mahospitali mengi na katika magereza miujiza hiyo inajionesha mara nyingi.

 Hakuna mtu ambaye hata kama aliishi vibaya , anaweza kuzuiliwa  neema yake. Tunajiwasjilisha mbele ya Mungu na  mikono mitupu, kidogo kama yule mtoza ushuru akiwa amesimama kwa  mbali bila hata kuinua macho yake mbinguni…( Lk 18,13). Baba Mtakatifu anashauri kuwa kila mtu anapofanya tathmini ya dhamiri  ya maisha yake binafsi akagundua  mapungufu wa mambo fulani ya matendo mema, basi asikate temaa, badala yake ni kuamini katika huruma ya Mungu.Anaongeza baba Mtakatifu, hiyo ndiyo inatupatia matumaini, ndiyo inayofungua moyo. Baba Mungu anasubiri hadi dakika za mwisho , na ndiyo maana mtoto mpotevu alipofika kwa Baba yake kuanza kuungama, baba yake alimfunga kinywa chake na kumkumbatia (Tz Lc 15,20). Huyo ndiyo Mungu na ndivyo atupendavyo.

Peponi siyo sehemu ya liwaya, wala bustani ya kustajaabisha. Peponi ni mkono wa Mungu anayekumbatia kwa upendo upeo, tunaingia humo kwa njia ya Yesu aliyekufa msalabani kwa ajili yetu. Mahali ambapo kuna huruma na furaha , bila yeye kuna baridi na giza. Wakati wa kifo  mkristo anamwambia Yesu; nikumbuke mimi. Iwapo hakuna hata moja anayekukumbuka, basi Yesu yuko pale anasubiri, yuko karibu nasi. Anataka kutupeleka katika sehemu nzuri iliyopo. Anataka kutupeleka  kwa kile kidogo au kikubwa cha wema kilichotendeka katika maisha yetu  kwamba ili hakuna lolote liweze kupotea. Katika nyumba ya Baba atapeleka kile ambacho bado tunahitaji: makosa yetu na maisha yetu yote ndiyo mwisho wetu wa maisha, kwani kila kitu kinapotea na kugeuka kuwa upendo tu.

Iwapo tunaamini hayo, Baba Mtakatifu anaongeza, tunaweza kushinda hofu za kifo,  tunaweza kuwa na matumaini ya kuondoka katika ulimwengu huu kwa utulivu na kwa matumaini.  Anayemjua Yesu, aogopi kifo tena. Tunaweza kurudia  hata maneno  ya mzee Simioni aliyebarikiwa katika kuonana na Kristo baada ya kuishi maisha yake yote akiwa na matarajio kwa kusema kwamba sasa bwana umetimizia ahadi yako, umruhsu mtumishi wako aende lwa amani , maana kwa macho yangu nimeuona wokovu (Lk 2,29-30). Baba Mtakatifu anamalizia akisema, kwa njia hiyo, wakati huo utakapotimilika  hatutakuwa na mahitaji yoyote , hatuchanganyikiwa , hakutakuwapo na kilio tena maana yote yamepita ,hata unabii maana ujuzi wetu si kamili na kipaji chetu cha kutangaza neno la Mungu si kamili, lakini kile kilicho kikamilifu kitakapofika vyote visivyo vikamilifu vitatoweka na upendo autakuwa na kikomo.

Mara baada ya katekesi yake Baba Mtakatifu amewakaribisha mahujaji wote  kutoka sehemu mbalimbali za dunia pia wanashirika wa Mitume wa Maria na wahudumu wa wagonjwa na mapadri Waeudisti. Amsema kufanya hija na kutembelea makaburi ya watakatifu iwe ni fursa yao ya kukua kwa upendo wa Mungu, ili jumuiya zao wanamoishi paweze kugeuka sehemu ya kufanya uzoefu wa umoja na huduma. Amewasalimia watu wa vyama mbalimbali, makundi ya maparokia kutoka sehemu mbalimbali za Italia na mwisho kuwasalimu vijana, wagonjwa na wanandoa wapya. Anasisitiza kuwa ni mwezi wa rosari na hivyo wakumbuke kusali rosari. 

Sr Angela Rwezaula 
Idhaa ya Kisahili ya Radio Vatican

 

25/10/2017 16:51