2017-10-24 09:46:00

Papa:Ujumbe wa Baba Mtakatifu kwa njia ya Video kwa Vijana wa Canada


Baba Mtakatifu ametoa ujumbe kwa vijana wa Canada kwa njia ya video iliyotolewa usiku wa Jumapili 22 Oktoba saa moja na nusu za usiku masaa ya Roma ikiwa Toronto ni saa moja  na nusu za Asubuhi ya tarehe 23 Oktoba 2017  na hiyo ni  katika tukio la maalumu la Televisheni nchini Canada iliyo andaliwa na Sel +Lumiere - Chumvi na Mwanga ili kuweza kuwasaidia Maaskofu wa Canada kuandaa Sinodi ya Vijana inayotarajiwa Oktoba 2018 yenye kauli mbiu “Vijana, Imani na  Mang’amuzi ya Miito ”.

Katika Studio ya Sel+Lumiere ( Chumvi na Mwanga) ya Toronto alikuwapo Kardinali Kevin Farrel , vijana , maaskofu wa miji sita ya Canada , ambao wameweza kuzungumzia juu ya changamoto , matatizo , maswali na mahitaji ya vijana wa Kanisa Katoliki.
Katika ujumbe wake, Baba Mtakatifu amewakumbusha kwamba, watu wanapofanya kazi pamoja wanafanya vizuri kwa ajili yao na hata kwa wengine na hivi ulimwengu unajionesha katika uzuri wake wote.

Ni Vijana wanaotoka katika miji sita ya Canada, Atlantiki hadi Pasifiki ambao wameshiriki pamoja na maaskofu wao wakiwa na Kardinali Kevin Farrel katika tukio la televisheni ambapo wamejadili changamoto, matatizo, maswali na mahitaji ya vijana katika Kanisa Katoliki ambapo Baba Mtakatifu amewaomba wasiache dunia iharibike kutokana na yeyote awazaye kujinufaisha nayo tu na kuiharibu.

Baba Mtakatifu anatoa wito na kuwaalika vijana kuzama kwa kina katika maeneo wanayoishi kwa furaha na shauku kubwa katika umri wwao, kuimarisha ulimwengu na historia kwa furaha ya Injili, na kuwa na Yesu aliyewavutia na kuwaita wawe naye. Halikadhalika anawahimiza vijana kuwa “Wafumaji wa mahusiano ya msingi na kuaminika, kusaidiana na uwazi mpaka mwisho wa dunia. Baba Mtakatifu pia anahimiza vijana kutokujenga kuta za migawanyiko! Anasema wajenge  madaraja, kama huu mkutano wao maalumu wanaofanya na kwamba ni jambo jema la kuunganisha mwambao wa bahari mbili, amesisitiza Baba Mtakatifu Francisko.

Akiendelea na ujumbe wake  anawakubusha vijana kwamba Yesu amekuwa wa kwanza kuwatafuta kila mmoja wao, akiwaalika wamfuate. “Nina hakika” anasema, ingawa inaonekana kuwa mshangao juu ya ulimwengu. Wito huu unaendelea kujiingiza katika nafsi yako ili kuifungua katika furaha kamili”.
Kanisa na Dunia  zinahitaji vijana shupavu, anasema Baba Mtakatifu na kuongeza, vijana wasio na woga mbele ya matatizo, walio tayari kuyakabili majaribu, wanaokaa macho na mioyo wazi juu ya uhalisia wa maisha kwa sababu hakuna atakayekataliwa iwe muathirika wa udhalimu, ukatili na kutothaminiwa kwa utu wa binadamu.

Baba Mtakatifu anahitimisha kwa  kuwaalika vijana wote kumwendea Yesu, na kukaa nae katika sala. Na amewaweka vijana wote chini ya ulinzi wa Maria wa Nazereti “Kijana kama nyie”: Mwacheni Maria awashike mkono na awaongoze katika furaha ya kujibu tazama “Mimi hapa” ambayo ni  thabiti  na kamili" anasema Baba Mtakatifu.

Frt Tito Kimario

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.