2017-10-23 17:00:00

Papa: Sayansi na Hekima lazima kutembea pamoja katika tafiti na ufundi


Ninawakaribisheni na kumshukuru Profesa Joseph Klafter,  Gombera wa Chuo Kikuu cha Tel Aviv, kwa maneno ya hotuba yake. Nawapongeza katika jitihada zenu za mafunzo kwa vizazi vipya , ambao wanawakilisha jamii ya sasa na ile endelevu. Shughuli za kufundisha pamoja na ugumu wake bado inabaki kuwa ni zoezi msingi ,makini kwasababu inalenga kumwandaa binadamu kamili.

Ni maneno ya Baba Mtakatifu Francisko, aliyo anza nayo kwenye hotuba yake alipokutana na Wajumbe kutoka Chuo Kikuu cha  Tel Aviv, Jumatatu 23 Oktoba 2017 mjini Vatican. Baba Mtakatifu anasema, ili kuweza kutimiza shughuli hiyo msingi lazima kwa thati kuwa na uwezo wa kitaamuluma, kiteknolijia, mbinu, hata  uwelewa na utu wema wa kibinadamu ili kuweza kuhamasisha mazungumzo ya kweli na wanafunzi na kuhimiza mafunzo yao wote, kama watu binafsi na kama wataalam wa baadaye katika maeneo yao ya utafiti.

Baba Mtakatifu anafafanua kuwa, sayansi na hekima vinapaswa kutembea kwa pamoja. Hekima kwa maana ya kibiblia inaweza kwenda zaidi ya upeo wa hali halisi ya ukweli ili kuweza  kujua maana ya mwisho. Chuo kikuu kinatakiwa kuelimisha utamaduni  ambao unaweza kuunganisha mbinu za kiufundi na kisayansi na zile za mwanadamu, kwa imani kwamba kufuata ukweli na wema ndiyo hatima ya kipekee. Salomoni mwana wa Daudi baada ya kuchaguliwa kuongoza, alikwenda kutoa dhabihu huko Gibeoni na kumtolewa Bwana maombi akisema, ninakumba unipe mimi mtumishi wako  moyo wa kusikia ili kuamua watu wako, niweze kutambua mema na mabaya ; maana ni nani awezaye kuhukumu watu wako walio wengi hivi? (1 Wafl 3,9).

Aidha Baba Mtakatifu akitumia maneno ya Hati ya Waraka kuhusu mazingira nyumba yetu (Laudato Si), anasema, dunia yetu ya sasa ina haraka na ulazima wa kupanua utamaduni wa hekima. Kuna ulazima wa kutafuta njia zinazofaa kuwandaa viongozi wenye uwezo wa kufungua njia mpya na  kujibu mahitaji ya kizazi cha sasa bila kuacha hata kile endelevu. (Taz: Barua. enc. Laudato si’, 53).

Hiyo ni lazima kwa sababu ya kuweza kutimiza haraka hii kwa namna ya pekee , ambayo ni muhimu kwa kufikiria hali halisi ya mageuzi na maendeleo ya ulimwengu unaokabiliwa na changamoto ya kipeo cha uchumi kijamii na migogoro isiyoisha. Baba Mtakatifu anasema kuwa anao  uhakika kwamba Chuo kikuu  kinatoa mchango wa kuwaandaa viongozi wapya, walio makini katika matatizo makubwa ya kimaadili ambayo yanatazam kwa karibu jumii zetu , aidha haraka ya kuhamasisha zaidi waleiwanaoathirika  ndugu zetu kaka na dada. Ni katika  kuhudumia maendeleo ya kibinadamu  kamili ya sayansi na maadili ya wanadamu inayoweza kujeleza heshima yao timilifu.

Amemalizia akiwashukuru na kuwatakia mafanikio mema na kwamba wanaweza kuwa daima na hekima ambayo ni zawadi ya Mungu inayowafanya wawe na  uwezo wa kuendesha  maisha yao mema na yeye kuzaa matunda,

Sr Angela Rwezaula 
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican








All the contents on this site are copyrighted ©.