2017-10-23 16:30:00

Papa: Oktoba 2019 umetangazwa kuwa mwezi maalumu wa Kimisionari


Tarehe 30 Novemba 2019 itakuwa ni siku ya kukumbuku ya kutangazwa kwa Barua ya kitume ya (Maximum Illud), mahali ambapo Papa Benedikto wa XV alipendelea kutoa uamsho kwa uwajibikaji kimisionari katika kutangaza Injili. Ilikuwa mwaka 1919 baada ya kumalizika kwa vita ya Kwanza ya dunia ambayo yeye binafsi alielezea kuwa  ni vita isiyo kuwa na  manufaa na kuonesha ulazima wa kuhamasisha Injili katika utume duniani hasa katika kusafisha vidonda na makovu vilivyokuwa vimesababishwa na ukoloni katika dunia.
Ni maneno ya Ujumbe wa Baba Mtakatifu Francikosko katika Barua aliyomwandikia  Kardinali Fernando FILONI Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya Unjilishaji wa watu.

Baba Mtaktifu Francisko katika barua hiyo anasema, Papa Benedikto XV aliandika, kuwa Kanisa la Mungu ni la ulimwengu mzima, halimpotezi yoyote na kuwataka wapinge kila aina yoyote inayokwenda kinyume manufaa ya  binadamu, badala yake wajikitike katika kutoa  habari njema na upendo ambao Bwana alisambaza kwa utakatifu wa maisha na matendo mema ambayo ndiyo sababu ya utume. Papa Benedikto XV kwa namna ya pekeealitoa  nguvu ya utume wa watu (Missio ad gentes katika matendo  na kwamba ni zana inayojikita kutoa habari njema katika enzi zile na kuwaamsha hasa makuhani waweze kuwa na utambuzi wa umisionari.

Ni  kujibu wito wa Yesu anayesema nendeni ulimwenguni kote na kutangaza Injili kwa kila kiumbe(Mk 16,15). Kukubali wito wa Mungu siyo uchaguzi tu wa Kanisa bali ndiyo wajibu wito wake kama anavyokumbusha na kusisitizwa na Mtaguso wa II wa Vatican, juu ya asili ya Kanisa kwamba, ni la Kimisionari: Uinjilishji ndiyo neema na wito wa Kanisa na utambulisho wake  wa kina.
Kujibu utambusho na kutangza Yesu msulimbiwa na aliyefufuka kwa ajili ya wote , mkombozi aliye hai, wa huruma, nayeokoa. Kanisa kwa maongozi ya Roho ya Kristo inajikita katika njia hizi za umaskini, utii, huduma na sadaka ya kujitoa binafsi. Ni kutangaza hali halisi ya Bwana kama mtindo wake  katika ubinadamu mpya kwa maana ya binadamu anayejionesha kindugukwa dhati na roho ya amani kwa wote.

Mtakatitu Yohane Paulo II, anaendelea Baba Ntakatifu Francisko, anaeleza kwamba, utume  wa Kristo uliokabidhiwa na Kanisa bado huko mbali kukamilika na ambao unamtazama moja kwa moja  binadamu ili kuonesha utume huo ambao bado ndiyo unaanza , kwa njia hiyo wote tunalazimika  kuweka jitihada na nguvu katika huduma yake. Baba Mtakatifu amependelea  kuwashauri kuwa makini  na kurudia upya kujikita katika huduma ya kimisionari wakiwa na uhakika kwamba utume wa Kanisa unaimarisha imani na utambulisho wa Kikristo,na kwa namana hiyo  Unjilishaji mpya wa watu utapata mwelekeo na msingi wa jitihada za kimisionari katika ulimwengu.

Barua ya Kitume ya Maximum Illud ilikuwa inaonesha roho ya kinabii kwa uwazi na unjilishaji wa kutoka nje katika kila kona ya mataifa kushuhudia mapenzi ya Mungu kwa njia ya utume wa kumisionari wa Kanisa katika ulimwengu.
Hivyo katika kukaribia mwaka wa miaka 100, uwe ndiyo chachu ya kushinda vishawishi vinavyojitokeza au kujificha nyuma ya kanisa, hasa ya kutaka  kujitokesheleza katika sehemu za giza,au kuonesha kila aina ya ugumu wa kichungaji, kila aina ya utasa au kumbukumbu za nyakati zilizopita, na ili kuweza kufungulia habari mpya ya furaha ya Injili.

Hata katika hali ya sasa mahali ambao kuna majanga ya vita matendo ya utofauti na migogoro, habari njema ya Yesu ya  msamaha unaoshinda dhambi, maisha yashinde kifo na upendo ushinde hofu kwa kila mmoja ili awe na matumaini na imani.
 Kwa njia hiyo kulingana na maombi ya Baraza la Kipapa la Uinjilishji wa Watu, Baba Mtakatifu anaelekeza mwezi maalumu wa Kimisionari Oktoba 2019 lengo lake ni kuwa na utambuzi zaidi wa Misio ad Agentes na kuanza upya mageuzi ya kimisonari katika maisha na katika uchungaji ulimwenguni 

Hiyo pia itaanza kuhamasishwa mwezi wa kimisonari Oktoba mwaka kesho ili waamini wote wawe kweli na moyo wa kutangaza Injili na uongofu wa Jumuia halisi ya kimisionari .

Sr Angela Rwezaula

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican








All the contents on this site are copyrighted ©.