2017-10-21 16:00:00

Papa:Ni vema uwepo wa makatekista katika nyumba za walemavu ili kuwasaidia


Baba Mtakatifu Francisko amekutana na wajumbe wa mkutano ulioandaliwa na Baraza la Kipapa la Uinjilishiji mpya mjini Roma. Katika hotuba yake, Baba Mtakatifu anampongeza Askofu Mkuu Rino Fisichella Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Uinjilishaji mpya kwa utangulizi wa hotuba yake, na  kwamba katika siku hizi za mkutano wamekabiliana na mada msingi, muhimu ya maisha ya Kanisa katika utume wa uinjilishaji na mafunzo ya kikristo hata katika nyanja ya watu wenye udhaifu kimwili. 

Utambuzi na  maendeleo makubwa kwa miaka hii ya mwisho umeweza kukabiliana  mapungufu. Kuongezeka kwa utambuzi wa maisha ya kila binadamu hasa wadhaifu, walemavu, umejikita kuchukulia  hatua za kijasiri kwa wale walio baguliwa na kuishi katika udhaifu ili kila mmoja asijisikie pweke au mgeni katika nyumba yake binafsi. Pamoja na hayo katika ngazi ya utamaduni bado kuna vielelezo vinavyojionesha kubezwa hadhi ya watu hawa ambao hawatambuliwi katika maisha ya kweli.

Baba Mtakatifu akichambua kwa karibu hali halisi ya watu walemavu anasema, kwa bahati mbaya kuma mtazamo wa  kutojali wa kuwaweka watu hawa kandoni, bila kupokea na kutambua aina nyingi za utajiri wa kibinadamu na kiroho walizo nazo. Na zaidi bado kuna ile tabia ya kubagua au kukataliwa hali ambayo humfanya mtu akose furaha na kujikamilisha mwenyewe.Kwa upande mwingine, ni udanganyifu wa hatari ya kufikiria kuwa hutukuathirika. Kama  alivyosema msichana aliyekutana naye wakati yuko safari ya kitume ya  hivi karibuni nchini Colombia, kwani kuathirika, kwa mujibu wa Baba Mtakatifu ni sehemu ya maisha ya binadamu.

 Anatoa mfano kuwa jaribio ambao linajitokeza wakati mwengine ni kujieleza kwa kiumbe anayezaliwa akiwa ulemavu. Wengi wetu tunao uzoefu ambao tumewahi kukutana na watu kama hao lakini pamoja na udhaifu  wanafanya kila njia na juhudi ambapo wameweza kupata njia bora ya kujikimu na yenye utajiri wa namna yake. Lakini pia tunaoutambuzi kuwa wapo watu wale ambao pamoja na kwamba ni wakamilifu, lakini bado wanahangaika ! Kwa njia hiyo jibu ni upendo,siyo udanganyifu , ni upendo wa kweli , wa dhati na kuheshimu. Mahali ambapo unahisi kupendwa, kupokelewa hawa wanaonao baguliwa katika jumuiya na kuwasindikiza kwa matumaini ya wakati ujao, kukuza mchakato wa kweli wa maisha na kufanya uzoefu wa furaha ya kudumu. 

Imani ni msindikizaji mzuri  wa maisha wakati ikituwezesha kugusa na kuonja uwepo wa Baba ambaye haachi kamwe viumbe wake kwa kila hali ya maisha.Kanisa haliwezi kufumba machao mbele ya kuhamasisha  ulinzi na uendelezaji wa watu wenye ulemavu. Ukaribu wake kwa  familia huwasaidia kuondokana na upweke ambao mara nyingi usababisha hatari ya kujifungia katika upweke huo kutokana na ukosefu wa msaada na uangalizi. Aidha baba Mtakatifu anasema katekesi kwa namna ya pekee ni kujikita zaidi kugundua na kufanya uzoefu wa aina mbalimba za dhati kwa kila mtu pamoja na zawadi zao, hata udhaifu wao wa kimwili walio nao, hata kama ni mkubwa wanaweza kukutana na Yesu katika njia na kujikabidhi kwake kwa imani.

Hakuna kikomo cha kimwili au kiakili kinachoweza kuwa kizuizi cha kukutana na Bwana, kwa sababu uso wa Kristo huangaza ndani ya kila mtu. Zaidi sisi pia tunapaswa kuwa makini, hususan wahudumu wa neema ya Kristo kutotumbukia  katika hilafu  na kutokuelewa  haja ya nguvu ya neema inayotokana na sakramenti hasa katika mchakato wa kuingia katika Ukristo.Baba Mtakatifu anasisitiza kuwa ni vema  kujifunza kushinda usumbufu na hofu ambayo wakati mwingine inaweza kujitokeza mbele ya uzoefu wa watu wenye ulemavu. Tujifunze kutafuta na hata kubuni  kwa  akili ili pasiwepo hata mmoja anayekosa neema hiyo. 

Aidha anatoa mfano  kwanza  makatekista wawe na uwezo wa kuongoza watu hawa kwa sababu wakue katika imani ili waweze kutoa mchango wao halisi na asili kwa  maisha ya Kanisa. 
Na mwisho Baba Mtakatifu anaonesha  matumaini ya kwamba kila jumuiya yenye walemavu inaweza kuwa na makatekista w kutoa ushuhuda kwao na kuonesha imani kwa ufanisi zaidi .


Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican








All the contents on this site are copyrighted ©.