Tarehe 20 Oktoba 2017, Baba Mtakatifu amekutana na Wanachama wa Taasisi ya Sayansi jamii na ubunifu wanaoshiriki katika mkutano wa mafunzo, pia hata taasisi zinazo wasaidia katika utafiti huo. Baba Mtakatifu anasema mafunzo hayo ni muhimu kwenye kipindi cha sasa cha dharura ili kuweza kujikita katika kutafuta na kubuni mbinu mpya za mshikamano katika soko, serikali na jamii ya umma ule uhusiano wa kukabiliana na changamoto za nyakati zetu.
Taasisi ya Yohane Paulo II iliundwa kwa lengo la kuhamasisha mafunzo na maendeleo ya Sayansi jamii, uchumi, siasa na sheria, ili kuweza kusaidia mambo msingi ya kutumia katika mafunzo na katika maendeleo ya mafundisho jamii ya Kanisa. Taasisi hiyo pia ina kazi ya kutafakari juu ya kuweka mafundisho jamii ya sasa. Kwa mujibu wa Baba Mtakatifu anaonesha kuwa ipo wasiwasi hata leo hii katika masuala makuu mawili msingi yanayosababisha kuongezeka ukosefu wa haki na ubaguzi wa maisha ya binadamu aliye pembezoni.
Ya kwanza anasema, ni ongezeko kubwa na mkakati wa kutofautiana na unyonyaji wa sayari kwa kiasi kikubwa kulinga na ongezeko la umaskini na matajiri. Hata hivyo yeye binafsi anasema, ukosefu wa usawa na unyonyaji sio uharibifu wala suala ambalo linajtokeza mara kihistoria. Siyo uharibifu kwasababu unasababishwa na mienendo tofauti kibinafsi na hata sheria za kiuchumi ambazo jamii uamua kutoa.
Sababu nyingine ya pili ni ile inyaohusu kazi isiyo faa kwa maisha ya binadamu. Anabainisha kuwa, kama jana Hati ya Kitume ya Rerum Novarum ya mwaka (1891), ilikuwa inatoa wito juu ya "bidhaa za haki" kwa ajili ya wafanyakazi. Leo hii bado kuna dharura kama ile ile ambapo ni suala la kujiuliza kwa nini haikuwekwa kwenye matendo kwa kile kilichoandikwa katika Waraka wa Mwanga wa Mataifa (Gaudium et spes) isemayo ni muhimu kukabiliana na mchakato mzima wa uzalishaji na mahitaji ya mtu na aina zake za maisha (n.67) Baba Mtakatifu nasema kuongezea tena Hati ya Kitume kuhusu “Sifa kwa Bwana ”(Laudato si) inayohusu mazingira kwa kuzingatia kazi ya uumbaji ambayo ni mazingira ya nyumba yetu .
Kwa mtazamo wa sehemu ya pili inayohusu ubaguzi wa kijamii , Baba Mtakatifu anatoa wito kuwa makini katika ulimwengu wa kazi ili kuweza kuwapo nafasi wazi, aidha kuwapo watu wenye uwezo wa kutengeneza mahusiano. Anawaalika kutoa vikwazo vitokanavyo na shinikizo la umma au kibinafsi ili kuweza kutetea maslahi ya sekta mbalimbali pia umuhimu wa kuondoa aina za uvivu kiroho. Hiyo inahitaji hatua za kisiasa zijikite kiukweli katika huduma ya binadamu kwa manufaa ya wote na heshima ya asili anasisitiza Baba Mtakatifu.
Maadili msingi kama vile demokrasia, haki, uhuru , familia, uumbaji haviwezi kutolewa sadaka na kuwa kama fadhili ya ufanisi , kwa kuwa njia pekee inathibitisha kwamba ni ustaarab wa soko. Baba Mtakatifu anabainisha: nchi au taifa, haliwezi kutambuliwa kuwa ni mmliki kwa manufaa ya wengine iwapo hairuhusu miili raia au jamii kuingilia kati na kujieleza kwa uhuru na kwa nguvu zao zote. Hii ni kuvunja kabisa msingi ambayo ni pamoja na mshikamano unaofanya nguzo muhimu ya mafundisho jamii ya Kanisa. Kwa njia hiyo Baba Mtakatifu anaonesha kuwa hapo kuna changamoto, jinsi gani ya kupatanisha haki ya mtu binafsi na ile ya faida kwa wote.
Mwisho anaonesha kutazama jukumu maalum ya vyama vya kiraia: kwamba, jukumu maalum la vyama vya kiraia ni kama kulinganishwa na kile cha Charles Péguy aliyejikita katika karama ya matumaini: kama dada mdogo kati ya fadhila nyingine mbili ya imani na upendo ikishikana mkono na kuvuta mbele yao. Kwa namna hiyo Baba Mtakatifu anasema jamii ya raia inapaswa kuvuta kwenda mbele ya serikali na soko ili kuweza kufikiri kwa upya sababu ya kuwepo na njia zao za kufanya kazi .
Sr Angela Rwezaula
idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican
All the contents on this site are copyrighted ©. |