2017-10-18 09:28:00

Wiki ya Afrika mjini New York inafanyika kuanzia 16-20 Oktoba 2017


Wiki ya Afrika kwenye Umoja wa Mataifa imeanza tarehe 16  hadi 20 Oktoba 2017, ambapo viongozi wa bara hilo wanakutana mjini New York, Marekani kujadili mafanikio na changamoto za bara hilo. Wiki ya Afrika ina lengo la mambo makuu muhimu ya  Kuunganishwa, Mafanikio na Watu wenye msingi wa Amani. Akizungumza na idhaa ya Umoja wa Mataifa  katika mahojiano maalum,  Afisa Mwandamizi kitengo cha mawasiliano, kamisheni ya uchumi Afrika Mercy Wamboi amesema dira wiki hii itajikita zaidi katika kutathmini utekelezaji wa ajenda ya 2063 ya maendeleo ya Afrika, sambamba na ajenda 2030 ya maendeleo  endelevu ya Umoja wa Mataifa.

Aidha meongeza watu waafrika watakuwa walengwa wakuu katika mijadala juma hili wakati wawakilishi wao na wadau wao wa maendeleo kutoka sehemu mbalimbali duniani wakikutana. Mijadala mathalani itajikita katika mpango wa mpya wa maendeleo barani Afrika, NEPAD unaojumuisha miradi kadhaa ya pamoja ya kikanda kama vile miundombinu, bila kusahau mpango wa bara la Afrika wa kujitathmini. Habari zaidi kutoka mtandao wa Umoja wa Mataifa walio andaa Wiki ya Afrika wanasema, Ajenda hizi mbili zinaimarisha  wakati huo huo wanazingatia mageuzi ya kimaumbile na endelevu katika vipimo vyote endelevu ikiwa ni pamoja na utawala, amani na usalama na maendeleo endelevu.

Bara la Afrika linalofanikiwa ni mojawapo ya kuona  uchumi tofauti wa kitaifa umeunganishwa na ushiriki kiuchumi na kijamii na kuhakikishiwa na kukuzwa kwa watu wote.  Serikali na wadau wakea  wanapaswa kufanya kazi ili kuhakikisha mazingira yenye rutuba ya ujasiriamali yanatoa mizizi na kustawi, na kuzuia ule  mtiririko wa kifedha usio halali, kama njia ya kuchochea ukuaji wa uchumi na kuzingatia amani na usalama. Washiriki wa maendeleo ya kimataifa, sekta binafsi na mashirika ya kiraia, na  kila mmoja huongeza thamani muhimu katika kuunga mkono matarajio ya Afrika. Matukio ya Wiki hii yanawakilisha fursa ya majadiliano ya wazi juu ya mada msingi kwa kauli mbiu hiyo.

Kwa ujumla, Wiki ya Afrika inaadhimisha na kuonesha  maendeleo ya Afrika na mafanikio yake kwa kuzingatia maendeleo ya kijamii, kiuchumi, kisiasa na mazingira. Wiki pia italeta ufahamu juu ya changamoto mpya zinazojitokeza kuikabili bara hilo  kwa lengo la kuhamasisha msaada wa kimataifa katika kiwango cha kimataifa na vipaumbele vya maendeleo ya Afrika na ajenda yake ya mabadiliko ya pamoja. Wiki ya Afrika ni tukio la kila mwaka lililopangwa pembeni mwa Mkutano Mkuu wa Mjadala juu ya maendeleo ya Afrika na Ofisi ya Mshauri Maalum wa Afrika (OSAA) kwa ushirikiano wa karibu na washirika wake wa kimkakati ikiwa ni pamoja na Mataifa wanachama.

Wakati huo huo tarehe 15 Oktoba 2017 ili kuwa ni Siku ya mwanamke wa kijijini.Ni siku ambayo huadhimishwa kila mwaka Oktoba 15. Katika ujumbe  maalumu kwa ajili ya siku hiyo mkurugenzi mtendaji wa shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya wanawake, Phumzile Mlambo Ngcuka amesema wanawake na wasichana ni kiungo muhimu cha maendeleo kijijini kuanzia katika familia zao hata katika jamii, kuboresha maisha ya kijijini na ustawi kwa ujumla lakini mara nyingi jukumu na umuhimu wao huwa unasahaulika.

Ukweli ni kwamba wanawake hao ni takribani nusu ya nguvu kazi katika mataifa yanayoendelea ikiwa ni pamoja na kuchukua sehemu kubwa ya ajira zisizo na malipo kama kutoa huduma na kazi za majumbani  katika familia. Bi Ngcuka ameongeza kusema, uelewa na ujuzi wao katika masuala ya uhakika wa chakula na lishe, ardhi na udhibiti wa maliasili unaongeza rasilimali katika kupambana na athari za mabadiliko ya tabia nchi. Amesema wanawake hawa wanalima sanjari na wanaume lakini hawafaidiki na mazao yao katika suala la bei, lakini pia wengi hawana fursa ya kumiliki ardhi, kupata mikopo, kuwa na sauti katika masoko na katika mfumo mzima wa chakula. Wanawake wa kijijini ni karibu robo ya watu wote duniani na wengi wa asilimia 43 ya wanawake wote ni wakulima.

http://www.un.org/en/africa/osaa/events/africaweek/

Sr Angela Rwezaula

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.