Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Habari \ Habari za Kimataifa

Calissita L. Giungrich ameteuliwa kuwa Balozi wa USA mjini Vatican

MS. Callista L. Gingrich ameteuliwa kuwa Balozi wa USA mjini Vatican. - AFP

17/10/2017 16:08

Senate ya Marekani imeridhia uteuzi wa Calissita L. Gingrich kutoka McLean kuwa Balozi mpya wa Marekani mjini Vatican. Balozi mteule amewahi kuwa Rais na Mkurugenzi Mkuu wa shughuli za uzalishaji za Kampuni ya Kimataifa ya Gingrich pamoja na kuwa mshauri wa Kampuni ya Arlington, yenye makao yake makuu mjini Virginia, nchini Marekani. Ni mwandishi maarufu sana wa vitabu na mtengenezaji wa sinema. Kwa muda wa miaka ishirini amekuwa ni mwanakwaya maarufu sana katika Madhabahu ya Kitaifa ya Kanisa kuu la “Immaculate Conception” Jimbo kuu la Washington DC. Ms. Calissta L. Gingrich amewahi kuwa msaidizi kwenye Bunge la Wawakilishi na Rais wa Mfuko wa Gingrich unaotoa msaada kwa ajili ya huduma ya upendo!

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.

17/10/2017 16:08