Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Kanisa Barani Afrika \ Amani

Sudan ya Kusini: Bado ni safari ndefu kuelekea haki, amani na hadhi

Jumatano 13 Oktoba Baba Mtakatifu alipokea nakala ya Kitabu cha Padre Daniele Moschetti kuhusu safari ndefu ya kuelekea amani, haki na hadhi - RV

16/10/2017 14:33

“Matukio yanayojitokeza nchi za kimaskini kama afrika, kwa bahati mbaya zinatolewa  kidogo, kwa mfano wa Sudan ya Kusini mahali ambapo ni kioo cha vyombo  vya habari  kutoa habari wanazopendelea lakini zaidi za  kuonesha majanga ya maelfu ya wanaokufa. Ni maneno ya Padre Daniele Moschetti Mmisionari wa Wakomboni, wakati wa kuwakilisha kitabu chake kwenye Studio za Radio Vatican , chenye kichwa cha habari “ Safari ndefu ya kuelekea amani,haki na hadhi” .

Ushuhuda wa Padre Moschetti unaonesha  kwa dhati hali halisi na juhudi nyingi za wamisionari katika nchi ya Sudan ya Kusini kutokana na kipeo cha vita kwa miaka hii. Padre Moschetti anasema, alipokutana na Baba Mtakatifu, ameonesha bado  shahuku ya kutaka kwenda  Sudan ya Kusini , mahali ambapo matatizo yao yako rohoni mwake.  Aidha amelezea juu ya uzoefu wake baada ya kukaa miaka 11 katika mtaa  kimaskini huko Korogosho nchini Kenya, pia kuanzisha baadhi ya mambo kadhaa kama vile, chama cha Wakuu wa Watawa wa Kusini mwa Sudan kwa kuunganisha kundi la Mashirika 43 Katoliki.

Padre Moschetti pia amekuwa mwanzilishi wa kituo cha Mchungaji Mwema katika kijiji cha Kit kilichoko mwanzo wa  Mji Mkuu Juba nchini Sudan.
Akiendelea na  maelezo kuhusiana na Sudan ya Kusini anasema Umoja wa Mataifa umefanya makosa  mengi katika nchi ya Sudan ya Kusini, lakini kwa ujumla hata Jumuiya ya Kimataifa kushindwa kuingilia kati kwa kina katika kutoa uamuzi wa kutosha katika nchi hiyo, mahali ambapo kuna maslahi kama vile ya mafuta ya petroli. 

Katika kuwakilisha kitabu hicho katika studio za Radio Vatican  chenye kichwa cha habari kuhusu safari ndefu kuelekea katika amani, haki na hadhi, kitabu hicho kina utangulizi wa maandishi ya Baba Mtakatifu Francisko akisema: “Ninahisi kuhamasisha jumuiya ya kimataifa katika janga la ukimya ambalo  linahitaji juhudi ya  pamoja ili kuweza kufikia hatma ya mgogoro unaoendelea. Kutojali matatizo ya kibinadamu katika muktadha wa mgogoro wa Sudan ya Kusini, ina maana ya kusahau somo litokanalo na Injili juu ya upendo wa jirani anayeteseka na kuhitaji”. Baba Mtakatifu anaongeza kusema “ kawaida  wamisionari wamezoeza  kusimulia maisha yao katika kuishi pembezoni na kwa upande wa maskini. Huo ndiyo ushuhuda wa ambao unajikita katika sehemu kubwa ya ukarimu na upendo mkuu wa juhudi za wamisionari wote wa kuwa karibu na wahitahiji zaidi wale wanaoteseka katika migogoro ya muda mrefu na kusababisha vifo na uharibifu".

Jumatano 13 Oktoba 2017, Padre Moschetti alimkabidhi Baba Mtakatifu  Francisko nakala ya kitabu chake, ambapo Baba Mtakatifu alirudia kumweleza juu ya shahuku ya kurudi kutembelea bara la Afrika kwa namna ya pekee Sudan ya Kusini. 
Padre Daniele Moschetti kuanzia Novemba 2017 ameteuliwa kufanya utume huko Marekani,  mahali ambapo ataendelea na shughuli za Sudan ya Kusini akiwakilisha kati ya Washington na New York, kufanya kama  daraja  kwenye  ofisi za Umoja wa Mataifa na Kongresi ya Marekani. Pamoja na hayo atakuwa anawasiliana na Mtandao wa Afrika kuhusu Haki na amani,  pamoja na wanashirika wenzake  wa kimisionari wa Mashirika mengine ya kidini.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 

16/10/2017 14:33