2017-10-14 13:46:00

Askofu Mkuu James Patrick Green kuiwakilisha Vatican nchini Finland


Baba Mtakatifu Francisko amemteua Askofu mkuu James Patrick Green, kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Finland. Ataendelea pia kuwa ni Balozi wa Vatican nchini: Denmark, Sweden na Iceland. Kabla ya uteuzi huu, Askofu mkuu Green alikuwa ni Balozi wa Vatican nchini PerĂ¹. Itakumbukwa kwamba, Askofu mkuu James Green alizaliwa kunako tarehe 30 Mei 1950 huko Philadelphia, nchini Marekani. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, kunako tarehe 15 Mei 1976 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre.

Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto kunako tarehe 17 Agosti 2006 akamteuwa kuwa Askofu mkuu na kuwekwa wakfu tarehe 6 Septemba 2006. Akatumwa kama Balozi wa Vatican huko Afrika ya Kusini, Namibia na mwakilishi wa kitume Swaziland na Lesotho. Tarehe 15 Oktoba 2011 akateuliwa na Papa mstaafu Benedikto XVI kuwa Balozi wa Vatican nchini Ugiriki hadi mwaka 2017 alipoteuliwa na Baba Mtakatifu Francisko kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Sweden, Iceland pamoja na Denmark.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.








All the contents on this site are copyrighted ©.