2017-10-13 16:16:00

Matendo ya upendo kwa ndugu ni nyenzo madhubuti dhidi ya shetani


Ni Yesu Kristo peke yake atakaye tuokokoa na mashetani wanaotufanya polepole tuangukie katika malimwengu pia kutokoa hata kwa mambo ya aibu na  ulaghai  ambao Mtakatifu Paulo anautaja katika kitabu cha Wagalatia. Ni maneno  ya Baba Mtakatifu Francisko asubuhi ya tarehe 13 Oktoba 2017 wakati wa mahubiri yake kwenye Kanisa la Mtakatifu Marta .

Baba Mtakatifu akitafakari Injili ya siku kutoka kwa Mwinjili Luka, Yesu anasema iwapo ninamfukuza Belzeburi kwa mkono wa Mungu, kwa maana hiyo wakati  wa ufalme wa Mungu umewafika. Baba Mtakatifu anatoa wito wa kufanya tafakari juu ya  dhamiri  hasa kujikita katika matendo  ndiyo yatatufanya tuwe wa kweli na ili wajanja na walaghai wasije ingia katika maisha yetu ambao  ni shetani.

Na Bwana anaomba kukesha ili kuhepuka kuingia vishawishi: kwa maana hiyo mkristo daima anakesha,  yuko makini kama walinzi. Injili inaelezea juu ya mapambano kati ya shetani  na Yesu, wakati wengine  wanasema  Yesu ana Belzeburi ili kuweza kufanya hayo yote aliyokuwa anatenda . 
Baba Mtakatifu anaenelea kusema, Yesu hasimulii historia tu, bali anasema ukweli: roho mbaya inapotoka katika binadamu inakwenda na kuzunguka katika jangawa ikitafuta mahali pa kutua, isipofanikiwa , inarudi mahali pale ilipotoka,mahali ambapo  ilikuwa inaishi kwa binadamu huru. 
Kwa maana hiyo ndiyo uamuzi wa  shetani kuleta marafiki zake wengine saba wabaya zaidi yake, kwa njia ya kufanya hali ya binadamu huyo aweze kuharibika zaidi ya kwanza. 

Baba Mtakatifu anaonya zaidi juu ya neno mbaya zaidi katika Injili kwamba ni kuonesha nguvu ya shetani anapoingia kwa binadamu na mabavu zaidi. 
Anafanya makazi ndani ya maisha ya binadamu,  katika mawazo yake ma  matarajio kwa kumfanya afikirie anaishi vema  na kumbe ameingiliwa katika moyo wake na kumbadilisha taratibu bila kufanya vurugu kubwa. Shetani anapoingia taratibu katika maisha yetu anabadilisha hata mantiki na kutupeleka katika malimwengu, na hiyo siyo rahisi zaidi kutambuakwa maana anakuja kiujanja sana Papa anabainisha. Na ndiyo hivyo binadamu aliyekombolewa , anaeuzwa na shetani na kua mkatili maana amejawa na malimwengu, hivyo ndivyo anavyotaka kuingia katika ulimwengu. Baba Mtakatifu anaonesha njia za ulaghai wa shetani  maana anapoingia katika maisha yake kwa shangwe anatumia upole, anatawala kila aina ya mtindo wa kuishi hata katika thamani zetu na juu kutoa huduma ya Mungu. 

Mkristo anageuka kuwa wa malimwengu, anakuwa wa uvuguvugu, anakuwa na mchanganyo katika roho kidogo ya malimwengu, na roho kidogo ya Mungu, lakini yote hayo mi kinyume na matakwa ya Mungu.Baba Mtakatifu anajibu swali ya jinsi gani ya kufanya ili kuhepuka hatari ya hiyo kwamba,  mada ya kuanguka katika vishawishi inawezekana kupingana bila kuogopa na kwa utulivu, ndiyo njia kubwa ya kuweza kuondokana na hira za shetani anayeingia taratibu katika maisha yetu.

Baba Mtakatitu anashauri njia za kufana kwamba, ni kukesha maana yake kutambua nini kinapita katika moyo, ni kutafakari na kufanya mang’amuzi ya maisha: nini maana ya kuwa mkristo?, ninajifunza au kuwafunza vema watoto? maisha yangu ni ya kikristo au ya malimwengu? Ninawezaje kutambua hilo? Na majibu yanatoka kwa Mtakatiff Paulo kuwa ni kutazama Kristo msulibiwa. Tunaweza kutambua hayo mahali ambapo msalaba wa yesu umefunjwa . Ndiyo lengo la Msalaba mbele yetu, msalaba siyo pambo tu. 

Ni msalaba unatukoa na ira za shetani ambaye anatuongoza tutmbukie katika malimwengu. Baba Mtakatifu anatualika kutazama Kristo msulibiwa, kwa maana  tunapofanya njia ya msalaba ni kutazama thamani kubwa ya wokovu na siyo tu kutazama dhambi bali  hata malimwengu.
Baba Mtakatifu anasisitiza kujitafuta dhamiri kuona ni kitu gani kinatokea katika maisha  . Lakini zaidi ni mbele ya Kristo Msulibiwa, Sala pia itakuwa vizuri  inasindikizwa na matendo ya upendo kwa ndugu,wagonjwa nakusaidia mtu aliye na shida. Hiyo ina maana ya kwamba matendo ya dhati yanavunja uhusiano unaotaka kufanywa na mashetani saba  wanaotaka binadamu atumbukie katika malimwengu.


 Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.