Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Baba Mtakatifu Francisko \ Hotuba

Ujumbe wa Papa kwa njia ya Video kwa miaka 300 ya Maria wa Aparecida

Baba Mtakatifu ametuma ujumbe wa kwa njia ya Video katika tukio la jubilei ya miaka 300 ya kupatikana kwa Sanamu ya Mama yetu wa Aparecida - RV

12/10/2017 17:01

Baba Mtakatifu ametoa ujumbe wake kwa njia ya video kutokana na maadhimisho ya miaka 300 ya kupatikana kwa Sanamu ya Bikira Maria wa Aparecida nchini Brazil. Na  katika  tukio hili BabaMtakatifu amemteua Kardinali Giovanni Battista Rei Mwenyekiti mstaafu wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya Maaskofu na Mwenyekiti mstaafu wa Baraza la Tume kwa ajili ya nchi za Amerika ya Kusini kumwakilisha katika maadhimisho ya miaka 300 ya kupatikana  kwa sanamu ya mama yetu wa Aparecida, ambaye ni msimamizi wa nchi ya Brazil, sikukuu inayofanyika katika Madhabahu ya Kitaifa ya Aparecida kwa siku kuanzaia 10-12 Oktoba.

Katika ujumbe wa video anaanza na salamu  kwa watu wote kuanzia viongozi wote wa Kanisa, na serikali ya nchi ya  Brazil wanaotoa ibada ya Mama Yetu wa Aparecida na msimamizi wa Brazil. Baba Mtakatifu anatoa salam zake na baraka maalumu kwa wote wanaoishi na Kristo katika Jubileia ya mwaka wa Maria kushehereka miaka 300 ya kupatika kwa sanamu ya mama huo kutoka katika mto wa Paraíba do Sul.
Katika tukio la ziara yake ya kwanza ya ya kitume kimataifa mwaka 2013 , Baba Mtakatifu anasema alipata furaha na neema ya kutembelea Madhabahu hayo  na kusali mbele ya sanamu ya Mama Maria akimkabidhi utume wake  wa kipapa na kukumbuka watu wa Brazil kwa makaribisho yao mema na moyo wao wa ukarimu. Katika tukio hilo,  Baba Mtakatifu anaongeza kuwa, alionesha upendeleo wa kusheherekea nao Jubilei hiyo, lakini maisha ya kuwa papa anasema  siyo rahisi.

 Kwa njia hiyo anasema amemtuma mwakilishi wake, Kardinali Giovanni Battista Re aweze kuadhimisha sherehe hizo tarehe 12 Oktoba 2017. Yeye amemkabidhi utume huo  wa kuhakikisha uwepo wa Baba Mtakatifu karibu nao. Aidha anasema pamoja na kutokuwapo kimwili,kwa bahati nzuri anaonesja shuhuku hiyo kwa njia ya Mtandao wa Mawasiliano wa  Aparecida  kuonesha ukarimu na upendo wa watu hao wenye ibada kuu ya Mama wa Yesu ambapo Baba Mtakatifu anatoa maneno rahisi yenye kutaka kuwakilisha uwepo wake kindugu katika sikukuu hiyo.

Akirudia maneno aliyo ya tamka mbele ya altare ya Madhabahu ya Kitaifa mwaka 2013 huko Aparecida , “tufungie na kutunza matumaini ili Mungu aweza kutoa mshangao na kuishi kwa furaha. Matumaini, kwa watu wa Brazil ni fadhila ambayo inapaswa kujikita zaidi katika mioyo ya wale wote wanao amini na zaidi  hasa katika kipindi kigumu na  misukosuko  na  mahali ambapo ni kujisikia kukata tamaa. Baba Mtakatifu anawashauri kuwa, wasikubali  kukata tambaa , wasikubali  kushindwa, wawe na matumaini  kwa Mungu,na matumaini kwa Mama yetu wa Aparecida,  Baba Mtakatifu anasisitiza. Katika madhabahu ya Aparecida na kila mwenye ibada ya Maria wote wanaeweza kuonja matumaini yanayo imarisha katika uzoefu wa kiroho, ukarimu , mshikamano, uvumilivu, na katika undugu, katika furaha vitu ambavyo ni vyenye thamani kubwa katika maisha na kujikita kwa undani mizizi yenye nguvu ya imani ya kikristo.

Katika mwaka  1717 kipindi ambacho wavuvi  majini  walikumbana na Sanamu  ya Mama Maria wa Aparecida , baba Mtakatifu anaongeza,  pale walihisi kuwa na imani kwa Mungu ambaye anatoa mshangao kwetu daima. Samaki kwa wingi na neema zilizotawanyika kwa namna halisi ya maisha ya wale ambao walikuwa wanamtegemea dhidi ya wenye nguvu. Mungu anatoa mshangao kwasababu  ni yeye aliye tuumba kwa upendo upeo  na anatushangaza daima. Katika kushereherekea jubilei ya miaka 300 ambapo Mungu anatoa mshangao , wote wanaalikwa kuwa na furaha  na shukrani.Furahisni katika Bwana daima (Fil 4,4). Furaha hiyo itokayo ndani ya mioyo yao inaweza kufikia kila kona ya nchi ya Brazil hasa katika maeneo ya pembezoni, kijamii na kuishi, kwa wale ambao kila wakati wanayo shahuku ya kuonja hata  tone la  matumaini hayo.
Tabasamu rahisi la Mama Maria  wanayojaribu kuiona katika uso wa picha, iwe ndiyo chemichemi ya tabasamu ya k la mmoja mbele ya matatizo ya maisha. Mkristo kamwe hawezi kuwa mgumu!

Anamalizia ujumbe huo akiwashikuru watu wote wa Brazil kwa ajili ya sala zao za kila siku anazo mwombea  hasa wakati wa maadhimisho ya misa, anasisitiza waendelee kusali kwa ajili yake, kama vile yeye anavyosali kwa ajili yao , kwa maana wote wawe karibu au mbali wanaunda Kanisa  na watu wa Mungu . Na kila wakati wanaposhirikiana kwa pamoja hata kwa njia rahisi lakini kwa dhati ni kutangaza Injili, ni kugeuka kuwa mashuda, kuwa wafuasi wa kweli na wamisionari. Leo hii nchi ya Brazili inahitaji wanaume na wanawake wenye kujawa na matumaini na imani thabiti, wawe mashuhuda wa upendo na kuonesha mshikamano, katika kushikirikishana na mambo yenye nguvu na mwanga katika giza la ubinafsi na ufisadi. Anawabariki na baraka ya kitume kwa maombezi ya Mama yetu wa Aparecida.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

12/10/2017 17:01