Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Baba Mtakatifu Francisko \ Hotuba

Ujumbe wa Papa kwa Miaka 100 ya Baraza la Kipapa kwa Makanisa ya Mashariki

Pamoja na utume unaotolewa na Chuo Kikuu cha Gregoriana na Taasisi ya Biblia, Baba Mtakatifu anasisitiza kuwa, kuna hata Taasisi ya Mashariki - AFP

12/10/2017 15:36

Katika maadhimisho ya miaka 100 ya Baraza la Kipapa kwa ajili ya Makanisa ya Mashariki, Baba Mtakatifu Francisko  ametoa ujumbe wake kwa ajili ya tukio hilo. Hawali ya yote kwa  Kardinali Leonardi Sandri, Mwenyekiti wa Baraza la Makanisa ya Mashariki, akiwatakia heri katika maadhimisho hayo  sanjari na maadhimisho ya  miaka 100 ya Taasisi  ya Mashariki ya Baraza hilo miezi michache iliyipita. Anampongeza yeye binafsi pamoja na jumuiya nzima ya taaluma. 

Baba Matakatifu anasema, nusu muhongo uliopita , Waraka wa mwongozo kwa Makanisa Katoliki ya Mashariki  papa laiyemtangulia  aliweza kuwa makini  kwa namna ya pekee  kuzingatia utajiri wa Makanisa ya Mashariki kwa kuanzisha mjini   Roma tarehe 15 Oktoba 1917, Baraza la Kipapa la nchi za Mashariki. Pamoja na kuanzishwa  Baraza hilo ndani ya Vita vya Kwanza vya Dunia , Baraza la kipapa liliendelea kujikita na shughuli zao kwa  Makanisa ya Mashariki kwa namna ya pekee. 

Katika tukio la kuanzishwa  kwake, Papa Benedikto wa XV alitoa wito wa ufunguzi  huko Mashariki Kongamano la Ekaristi huko Yerusalem mwaka 1893 , kwa  matumaini ya kuunda pia kituo cha mafunzo ambayo yangeweza kuwa baadaye  na  Hati ya ufunguzi wa kituo cha masomo ya juu yanayohusu mambo ya Mashariki, kwa ajili ya kuwalea mapadre hata wa Roma ambao wangeweza  kutoa huduma ya kikuhani katika nchi za Mashariki. Mwanzo Taasisi  hiyo walitaka ifunguliwe hata nchi za Mashariki kwa kuunganisha  kama isemavyo Orthodox  lakini wakati huo huo ikiwa inafanana na Mafundisho  Katoliki na yale ya. Kwa uhakika na  kwa  maneno rahisi , mwanzilishi alitaka kufungua Taasisi kwa mtazamo ambao leo hii ndiyo ule wa kiekumene.
Ili kuweza kutatua matatizo, mwanzo Taasisi ya Pio XI kwa kufuata ushauri wa Mkuu wa  chuo , Mwenye heri Ildefons Schuster, mwaka 1922 aliamua kuwakabidhi Chuo hicho, Shirika la Wayesuit  karibu na Kanisa Kuu la Mtakatifu Maria Mkuu tarehe 14 Novemba 1926.

Kwa Waraka wa kitume  kuhusu maisha ya Makanisa  Katoliki ya nchi za Mashariki uliotolewa tarehe  8 settembre 1928,  Papa Pio XI aliwaalika   maaskofu wote  watume wanafunzi katika Taasisi ya Masomo ya Mashariki ili kuwahakikisha kuwa kila seminari inakuwa na mwalimu mtaalaam wa mafundisho yanayohusu  nchi za Mashariki. Na kwa hati yenyewe ndipo wakaunganisha na Chuo Kikuu cha Gregoriani na kuzindua  Taasisi ya  Biblia na masomo ya Mashariki.  Mwaka ulifuata Papa Pio akaunda mkabala Taasisi nyingine ya Mashariki itwayo  Russicum mahali ambapo aliwapa  Shirika la Wayesuit tena  kuwa wasimamizi .

Baba Mtakatifu anaendelea na historia hiyo mwaka  1971 kukawa na habari njema ya kuanzishwa kwa taaluma ya mafunzo ya Sheria ya mashariki hadi sasa inaendelea lakini kwa muundo mpya, ijulikanayo Sayansi ya Makanisa ya Mashariki , inayogawanyika katika sehemu tatu:  taalimungu,  mafunzo ya mababa wa Kanisa, Liturujia na Historia. Jambo muhimu   jipya lilitokea tena  mwaka 1993  ambalo ni kuhamisha jina la Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa kwa ajili Elimu Katoliki na kuwa Mwenyekiti wa  Baraza la Kipapa kwa ajili ya Makanisa ya Mashariki. Taasisi hizo kwa pamoja  ni kuendelea  katika kuhamasisha mshikamano na umoja katika huduma ya wakristo wa mashariki.

Baba Mtakatifu anafafanua zaidi kuwa, iwapo mwanzo wake  kidogo kulikuwa na matatizo  na misukosuko kati ya masomo na uchungaji , leo hii hayapo tena Baba Mtakatifu anathibitisha , hakuna tena matatizo hayo, kwa njia hiyo anawaalika wakunfunzi wote kuweka kipaumbele zaidi katika juhudi zao za utafiti kisayansi kwa kuiga mifano ya watangulizi wanalio weza kutoa mchango mkubwa wenye thamani kuandika vyanzo vya kiliturujia, kiroho, kisanaa na matoleo mbalimbali ya mafunzo juu ya nyaraka mbalimbali za mwongozo wa Kanisa Katoliki la Mshariki na Waraka juu ya Uekumene, baadaye ukafutia maandalizi ya Gombo la Sheria ya Makanisa ya Mashariki 1990.

Pamoja  hayo siku za sasa tunazoishi na changamoto za vita chuki zinapelekea mizizi ya halisi ya kutafuta amani  kwa watu wanaoishi  katika nchi za Mashariki ambao kwa mara nyingine tena ni kama miaka 100 iliyopita. Kwa kutunza umakini na kuendeleza utafiti wa asili,  Baba Mtakatifu anawalika kuendelea kutoa ushuhuda katika Makanisa na jumuiya zote za kanisa,  ule uwezo wa kusikiliza  katika maisha na kutafakari kitaalimungu , ili kuweza kusaidia safari yao ya kuishi. 

 Wanafunzi wengi na walimu, wanahisi juu ya kipindi hiki muhimu cha kihistoria. Taasisi  kwa njia ya  kujikita katika utafiti, mafundisho , ushuhuda , wanayo kazi ya kuwasaidia ndugu na kaka wanaoteseka kwa kuwatia nguvu na juhudi, kuwaimarisha katika imani yao mbele ya changamoto wanazokumbana nazo. Aidha  Taasisi inaitwa kuwa sehemu mwafaka wa kusaidia mafunzo ya waume na wake, waseminari, mapadre na walei, ili kuweza kutoa sababu ya kweli ya matumaini yao na uwezo wa kushirikiana katika utume wa Kristo.

Baba Mtakatifu anawataka wakufunzi  wazidi kufungulia Makanisa ya mashariki na siyo kufukiria tu katika enzi za kale , bali katika hali halisi ya sasa . Uwepo wa mahusiano ya Makanisa ya Mashariki hadi sasa ni ile safari ya kweli ya kufikia umoja ambao ndiyo njia hiyo  ya kutembea  inayoonekana katika  Baraza la Kikapa la Mashariki na  utume wa kiekumene unao endelea mbele.

Kwa upande mwingine ni vema Taasisi kuwafanya kutambua tunu na utajiri wa tamaduni za Makanisa Mashariki ili kwamba wanafunzi waweza kuwelewa vizuri na kufananisha kwao. Kila wakati wapo wanafunzi wengi katika Taasisi za mashariki zilizoko Roma Baba Mtakatifu anasema,na wengine katika vyuo vya kipapa wanapokea mafunzo  japokuwa mengine hayaendani na tamaduni zao asili, kwa njia hiyo anawashauri Baba Mtakatifu kutafakari hili ili kuweza kutoa pengo hilo.

Kwa upandewa Shirika   la Wajesuit, Baba Mtakatifu Francisko anatoa wito leo ya kuwa wawe na  utambuzi wa hali halisi kwa kutazama maombi yaliyotolewa mwaka 1928 Papa Pio XI kuhusu Chuo Kikuu  Gregoriani, kilichokuwa kimeanzishwa  kwa namna ya pekee kwa  watu na chombo kukubwa cha umoja. Pamoja na utume unaotolewa na Chuo Kikuu cha Gregoriani na Taasisi ya Biblia, Baba Mtakatifu anasisitiza kuwa, kuna hata Taasisi ya Mashariki inayopaswa kutambuliwa kwa wote. Kuna umuhimu wa kuhakikisha  Taasisi hiyo inakuwa thabiti kwa walezi wa Kijesuit ambapo wengine wataweza kuwasadia wengine. Inatoa mafunzo  ya Mtakatifu Iginatius inayohusu mang’amuzi na kuishi kijumuia ikiwa pia taalimungu, wote wataweza kusaidia katika haraka ya kichungaji mahali ambapo Kanisa litawahitaji.

Baba Mtakatifu Francisko anaungana kikamilifu katika maadhimisho ya miaka 100 ya Taasisi ya Kipapa mashariki  kuendelea na juhudi ya utume, katika kusambaza upendo, ukarimu wa kitaaluma na kisayansi katika mtazamo wa uchungaji asili katika Makanisa ya Mashariki, kiliturujia, teolojia, mafunzo ya mababa wa Kanisa, sheria kwa kujibu vema wito wa  shughuli za Kanisa zinazohitajika katika ulimwengu leo hii na kutka ulimwengu wa amani na mapatano endelevu.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 

12/10/2017 15:36