Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Vatican \ Hotuba

Wafuasi wa Papa katika mtandao wa kijamii twitter ni zaidi ya millioni 40

Kila siku kwa njia ya Tweet za Baba Mtakatifu Francisko, anakuwa karibu na binadamu hata katika vyombo vya habari na mitando ya kijamii wakati mwingine akitoa neno la kiroho na kukumbuka Mtakatifu wa siku, - AFP

11/10/2017 16:48

Mtando wa Baba Mtakatifu wa Twitter  wenye lugha 9 kupitia @Pontifex umezidi zaidi ya milioni 40 ya wafuasi wakea (follower). Takwimu hizo ni kwa mujibu wa Sekretarieti ya Mawasiliano ya Vatican , ambayo imetoa taarifa hizo wiki chache kabla ya  kufikia mwaka wa tano tangu ufunguzi wa  mtandao wa papa ulioanzishwa  tarehe 12 Desemba 2012 kwa utashi ya Baba Mtakatifu Mstaafu benedikto wa XVI. Kila siku kwa njia ya Tweet za Baba Mtakatifu Francisko, anakuwa karibu na binadamu hata katika vyombo vya habari na mitando ya kijamii wakati mwingine akitoa neno la kiroho na kukumbuka  Mtakatifu wa siku, wakati mwingine kushirikishana na wafuasi wake tafakari juu ya matukio makubwa na yenye maana kwa ajili ya jumuiya ya kimataifa.

Kufutilia mbele ya neno la wafuasi wa papa katika Twitter , hawakupungua kamwe kwa  miaka hii, kwa maana katika miezi 12  wafuasi wake wameongezeka zaidi ya milioni 9 na kuonesha kufutilia kwa umakini wa watu wa kawada, wakristo na wasio wakristo, viongzoi wa kisiasa  na hata wengizine katika utamaduni kufuatilia Tweet za Baba Mtakatifu.

Uwepo mstari wa mbele katika mitandao ya kijamii,ya baba Mtakatifu unasindikizwa na idadi kubwa ya ujumbe juu ya utume wa wakristo katika bara la digitali. Katika tukio la Ujumbe wake wa kwanza kwanye Siku ya Dunia ya Mawasiliano ya kijamii iliyotangazwa tarehe 24 Januari 2014 , baba Mtaktifu anasisitixa kuwa mtando wa kidigitali unaweza kuwa sehemu yenye utajiri wa kibinadamu , na siyo mtandao wa waya  bali wa binadamu.Kuhusisha mtu ndiyo mzizi wenyewe wa kuamini katika kuawasiliana. Na kwa njia hiyo ushuhuda wa kikristo kwa njia ya mtandamo unaweza kufikia hata sehemu za maisha pembezoni 

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 

11/10/2017 16:48