Leo nataka kusimamia juu ya ukubwa wa matumaini ambao ni kuwa tayari na subira. Mada ya subira ni mojawapo ya mwongozo wa Agano Jipya. Katika mahubiri ya Yesu kwa wafuasi wake aliwambia muwe tayari mmejifunga mikanda kiunoni na taa zenu ziwe zinawaka muwe kama watumishi wanao mngojea Bwana wao arudi kutoka harusini ili wamfungulie mara atakapo bisha » (Lc 12,35-36). Ni maneno ya tafakari ya Baba Mtakatifu Francisko wakati wa katekesi yake ya Jumatano 11 Oktoba 2017 katika viwanja vya Mtakatifu Petro akiendelea na mfululizo wa tafakari za matumaini ya Kikristo. Baba Mtakatifu anasema, katika kipindi baada ya ufufuko wa Yesu ni hali inayoendelea wakati mwingine ya matukio ya faraha na uchungu lakini wakristo wasijisahau kamwe. Injili inasisitiza kuwa, wawe kama watumishi wasio lala usingizi mpaka atakapofika Bwana wao. Na hiyo inadhihirisha ni jinsi gani ya mkristo anapaswa kuwajibika na jisni gani ya kutimiza hayo katika maisha yetu yote.
Yesu anataka maisha yetu yote yawe ya kuwajibika bila kuchoka na kutoa shukrani kwa maajabu yake tunayo pokea kila siku. Kila asubuhi ni ukurasa mpya mweupe ambao mkristo analazimika kuandika matendo mema. Sisi tumekombolewa tayari na Yesu, lakini sasa tunasubiri ukamilifu wa maonesho hayo ya ukuu wake mahali ambapo Mungu atakuwa ni wa watu wote na kila kitu. Lakini kakuna mwenye uhakika wa siku hiyo katika imani ya mkristo, Baba Mtakatifu anasisitiza, siku ya Bwana atakapokuja hakuna hajuaye , lakini siku hiyo takapokuja wakristo wote wawe tayari kupokea ukombozi ambao tayari unawafikia.
Baba Mtakatifu ameuliza swali kwa wote walio udhuria katekesi hiyo katika viwanji
vya Mtakatifu Petro, iwapo wako tayari kukutana na Yesu atakapokuja. Lakini siku hiyo
itakuwa ni ya furaha kubwa na kukumbatiwa kwa furaha , hiyo ndiyo kukutana na Bwana,
ni lazima kuishi kwa subira ya kukutana.
Akifafanua na kutoa mfano Baba Mtaktifu anasema, mkristo hakuumbwa kuwa mvivu au kukosa
uvumilivu . Japokuwa anatambua kuwa uvuvi unaojitokeza wakati mwingine una manufaa
na umejifunika katika fumbo la neema. Kuna watu ambao wanavumilia kwa upendo ba
daaye hugeuka kuwa kisima cha kumwagilia jangwa. Hakuna chochote kitokachopotea ,
hakuna hali ambayo mkristo anakumbana nayo na isiwe na upendo mkamilifu. Hakuna usiku
mrefu wa kufanya usahahu furaha ya machweo.
Kadiri inavyozidi kuwa usiku wa giza nene ndipo likaribia kuchomoza jua.Iwapo tunabaki
tumengana na Yesu hasa katika ubaridi wa kipindi kigumu tusiwe kiwete, hata kama
ulimwengu utatangaza kupambana dhidi ya matumaini, hata wakisema wakati ujao utakuwa
ni mawingi meusi , mkristo anatambua vema kuwa wakati ujao yupo Kristo atakayerudi
tena. Je ni lini itatokea , hakuna anayejua, siku wala saa, lakini mwisho wa historia
ya maisha yetu yupo Yesu wa huruma, inatosha kuwa na matumaini na siyo kulaani maisha.
Kila kitu kitakombolewa anasema Baba Mtakatifu.
Yote upata mateso anaendelea, kutakuwa na kipindi cha kukasirika na ghadhabu, lakini
cha muhimu ni kukumbuka kuwa Kristo atafukuza vishawishi vya kufikiria na juu hisia
za kukosea maisha. Hiyo ni baada ya kumtambua kristo na kufikiria historia ya imani
na matumaini. Yesu ni kama nyumba ambayo sisi tumo ndani yake na madirisha yake
ndipo tunatazama ulimwengu kwa nje . Kwa njia hiyo hatuwezi kujifungia ndani sisi
wenyewe , hakuna kulia kwa uchungu kwa yale yaliyopita. Ni kutamani daima kwenda mbele
na maisha endelevu ambayo hayatengenezwi kwa mikono yetu zaidi ni Mungu mwenyewe
anayehangaikia watu wake . Baba Mtakatifu ansisitiza, kila kitu katika giza kitakuwa
na mwanga!
Ni lazima kufukiria kuwa Mungu hajidanganyi mwenyewe . Kamwe hadanyi! Mapenzi yake kwa ajili yetu hayana mawingu meusi, bali analinda na kuokoa moja kwa moja, kama asemavyo Mtakatifu Paulo kuwa, Mungu anataka watu wote waokolewe na wapate kujua ukweli (1Tm2,4). Kwa njia hiyo hatuna haja ya kujiingiza katika matukio yenye ugumu , utafikiri ni kama historia ya treni iliyopotea usikuni wake. Kukata tamaa siyo fadhila ya kikristo. Na pia siyo Ukristo wa tabia ya kugeuza mabega, kwa maana kila mkristo lazima awe jasiri na kujihatarisha kwa ajili ya wema wa wote, kama vile Yesu ambaye alitupatia wema huo na kuwa tunu msingi wa maisha yetu.
Kila siku katika maisha yetu , turudie kuomba kama wafuasi wake wa kwanza kwa lugha ya kiaramaiko waliosema ”Maranatha" maana yake, "Uje Bwana Yesu" (Rej: Uf 22,20) Ni kiitikio cha wakristo wa kila muhongo na katika ulimwengu wetu wetu wenye kuwa na mahitaji ya huruma ya Yesu .Katika sala zetu wakati wa kipindi kigumu tuweze kusikia sauti inayojibu Tazama mimi naja upesi (Rej: Uf 22,7).
Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican
All the contents on this site are copyrighted ©. |