2017-10-11 16:35:00

Papa: Akubali ombi la kuwatangaza wenye heri watumishi wa Mungu


Tarehe 9 Oktoba Baba Mtakatifu Francisko  amekutana na Kardinali Kardinali Angelo Amato, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya Mchakato wa kuwatangaza wenye heri na Watakatifu, wakati wa mkutano wao, amekubali kuwatangaza wenye heri watumishi wa Mungu Tullio Maruzzo Padre wa Shirika la ndugu wadogo Wafranciskani na Luigi Obdulio Arroyo Navarro, Msekulari wa Shirika la Mtakatifu Francisko, walio uwawa kwa ajili ya imani yao tarehe 1 Julai 1981 huko Los Amates nchini (Guatemala).

Mtumishi wa Mungu  Donizetti Tavares wa Lima, padre wa Jimbo alizaliwa  tarehe 3 Januari 1882 huko Cássia (Brasile) na kifo chake tarehe   16 Juni 1961 huko Tambaú (Brasile); Mtumishi wa Mungu Serafino Kaszuba padre wa Shirika la ndugu wadogo Wakapuchini. Alizaliwa  tarehe  17 Juni  1910 huko Zamarstynów, karibu na  Lviv (Ucraina) kifo chake tarehe 20 Septemba 1977 huko Lviv (Ucraina);
Mtumishi wa Mungu Magín Morera y Feixas, padre wa Shirika la Familia Yesu Maria na Yosefu. Alizaliwa tarehe  16 Novemba 1908 huko Sant Matu de Bages (Spagna)  kifo chake tarehe 28 Juni 1984 huko Barcelona (Spagna);

Mtumishi wa Mungu  Maria Lorenza Requenses in Longo,  Mwanzilisho wa Hospitali ya magonjwa sugu huko Napoli wa Shirika la watawa wa kike Wakapuchini. Alizaliwa  1463 huko  Lleida (Spagna) na kifo chake terehe 21 Desemba 1539 huko Napoli (Italia);
Mtumishi wa Mungu Francesca wa Roho Mtakatifu Mwanzilishi wa Shirika la waseculale wa Mtakatifu Francisko wa  Montpellier; alizaliwa tarehe  12 Desemba 1820 huko Mailhac (Francia) kifo chake tarehe 28 Decemba 1882 huko Saint-Chinian (Francia);

Mtumishi wa Mungu Elisabetta Rosa Czacka, Mwanzilisho wa Shirika la kitawa la Wafransiscani wa tumishi Msalaba. Alizaliwa tarehe 22 Oktoba  1876 huko Biała Cerkiew (Ucraina) na kifo chake tarehe  15 Mei  1961 huko Laski (Poland);
Mtumishi wa Mungu Francesco Paolo Gravina, Mlei na Mwanzilishi wa Shirika la Watawa wa upendo wa Mtakatifu Vincenzo de Pauli. Alizaliwa tarehe 5 Februari  1800 huko Palermo (Italia) na kifo chake 15 Aprili 1854 huko Palermo (Italia).

Sr Angela Rwezaula

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.