2017-10-11 16:23:00

Papa:13 Oktoba ni siku ya kupunguza majanga ya asili duniani mwaka 2017


Ni kuhamasisha utamaduni wa kupunguza hatari zinazohusiana na majanga ya asili. Ni maneno aliyosisitiza Baba Mtakatifu Francisko mara baada ya Katekesi yake kwenye uwanja vya  Mtakatifu Petro na kutoa wito. Aidha amewakumbusha tarehe 13 Oktoba  kuwa ni siku ya kupunguza majanga ya asili duniani kwa mwaka 2017 yenye malengo saba ya Kampeni “Sendai Seven”.

Majanga ya asili yanajitokeza mara kwa mara kutokana na mabadiliko ya tabia nchi kwa njia hiyo, Baba Mtakatifu anatoa wito kwa moyo wote kwa ajili ya kulinda kazi ya uumbaji kwa umakini na uangalifu wa mazingira. Anawatia moyo Taasisi zote wadau wote na wote wenye majukumu ya umma na kijamii kuhamasisha na kukuza utamaduni zaidi. Hatua halisi ambazo zinahitajika ni kujifunza na kulinda mazingira yetu ambapo inawezekana kupunguza hatari kwa watu wanaoishi katika mazingira magumu zaidi.

Aidha kama kawaida yake  Baba Mtakatifu ametoa salam kwa wahujaji kutoka pande zote za dunia  akiwatakia matashi mema ya kutembelea kaburi la Mtakatifu Petro kuwa, wapate uzoefu na kuimarisha imani yao na kushiriki katika familia ya Kanisa na kuhamasisha zaidi huduma kwa ukarimu na ujazo wa matumaini. Aidha amewakumbusha kuwa mwezi wa kumi ni mwezi wa Mama Maria ambao pia ni mwezi wa kimisionari. Wakumbuke wote kusali Rosari kwa mama wa Maria wa wamisionari.

 Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.