Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Baba Mtakatifu Francisko \ Hotuba

Ratiba ya Ziara ya Baba Mtakatifu huko Myanmar na Bangladesh kutolewa

Imetangazwa rasmi ratiba Ziara ya Baba Mtakatifu Francisko huko Myanmar na Bangladesh kwenye. Ziara yake inatarajiwa kuanza tarehe 26 Novemba hadi 2 Desemba 2017. - ANSA

10/10/2017 16:29

Tarehe 10 Oktoba 2017 imetangazwa rasmi  ratiba  ya Ziara ya Baba Mtakatifu Francisko huko Myanmar na Bangladesh kwenye Vyombo vya habari Vatican. Ziara yaae inatarajiwa kuanza tarehe 26 Novemba hadi 2 Desemba 2017. Baba Mtakatifu atawasili Bangladesh Jumapili ya tarehe 26 Novemba karibia saa 4 za usiku masaa ya Ulaya.  Tukio la kwanza huko Myanmar atapokelewa rasmi uwanja wa kimataifa wa ngedu Yangon, jumatatu 27 Novemba saa saba na nusu mchana. 

Siku itakayofuatia huko  Nay Pyi Taw atapokelewa kwenye nyumba kuu ya  Rasi mahali ambapo  atakutana na vingozi mbalimbali wa nchi, mchana atahututubia kwa umma na viongozi wa kidiplomasia badaye kurudi na ndege huko yangon.
Jumatano asubuhi 29 Novemba Baba Mtakatifu ataadhimisha misa takatifu  huko Kyaikkasan Groun huko Yangon. Mchana anatarajiwa kufanya mikutano miwili: kwanza na baraza la kuu la Sangha ambalo ni Jumuiya wa Wabudha , mkutao wa pili ni kukutana na  maaskofu wa nchi katika Kanisa kuu la Mtakatifu Maria.

Alhamisi 30 Novemba, Baba Mtakatifu ataadhimisha misa kwa vijana katika Kanisa la Mtakatifu Maria na  mchana ataondoka kuelekea Bangladesh .Baada ya sherehe fupi za makaribisho katika uwanja wa kimataifa katika mji mkuu wa Dhaka, Baba Mtakatifu atatembelea Jumba la makumbusho la kitaifa la Sava mahali ambapo ataweka shahada la maua kuenzi baba wa Taifa Bangabandhu.

Saa kumi na mbili za jioni ya masaa ya huko atahutubia mbele ya viongozi wote wa nchi, raia na viongozi wa kidiplomasia.
Ijumaa tarehe 1 Desemba 2017 atakuwa na mikutano minne ya nguvu: misa ya kutoa daraja takatifu la mapadre , kutembela Kanisa Kuu, kukutana na Maaskofu wa Bangldesh na mkutano wa kidini na kiekumene kwa ajili ya amani. 

Tarehe 2 ni siku yake ya mwisho ya ziara  ambapo  Baba Mtakatifu atafanya ziara fupi binafsi katika nyumba ya mama Tersa wa kalkuta huko Tejagon, mahali ambapo atakutana na wapadre na vijana wa Chuo cha Mama yetu huko Dhaka. Anatarajia kuanza safari ya kurudi saa 11 za jioni masaa ya huko , na kuwasili mjini Roma majra ya usiku sana.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 

 

10/10/2017 16:29