Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Baba Mtakatifu Francisko \ Hotuba

Baba Mtakatifu amekutana na Rais wa Ujermani Bwana Steinmeier

Baba Mtakatifu amekutana na Rais wa shirikisho la Jamhuri ya Ujerman, Bwana Franck-Walter Steinnmeier tarehe 9 Oktoba 2017 mjini Vatican - ANSA

10/10/2017 09:07

Hali ya  uchumi na dini barani Ulaya na katika ulimwengu,matukio ya wahamiaji na uhamasishaji wa utamaduni wa kukaribisha na mshikamano. Ni baadhi ya masuala muhimu yaliyozungumzwa asubuhi ya tarehe 9 Oktoba 2017 mjini Vatican, Baba Mtakatifu na Rais wa Shirikisho la Jamhuri ya Ujermani, Bwana Franck-Walter Steinmeier. Mara baada ya mkutano huo amekutana na Katibu wa Vatican Kardinali Pietro Parolin, akisindikizana na Katibu mkuu wa mambo ya nchi za nje na ushirikiano wa kimataifa mjini Vatican Askofu Mkuu Paul Richard Gallagher. Katika mazungumzo yao wameonesha furaha kuhusu uhusiano mwema na  mshikamano kati ya Vatican na nchi ya Ujerumani,  kati ya Ujerumani na Makanisa na Taasisi mbali mbali za kidini nchini humo. Pongezi pia zimetolewa kutokana na  majadiliano ya  kidini na kiekumene kwa namna ya pekee kati ya wakatoliki na waluteri hasa katika maadhimisho ya miaka 500 ya Mageuzi ya Kiluteri Duniani.

Baada ya mkutano huo na Baba Mtakatifu, Rais Steinmeier alikutana na waandishi wa habari na kuacha mahojiano kuhusu mkutano huo ambapo Rais anasimulia kushangazwa na utu wa Baba Mtakatifu, mtindo wake wa  uwazi na usikivu wa makini. Wamezungumza juu ya hali halisi ya nchi yake ya  Ujermani mara  baada ya uchaguzi. Rais anadai kuwa, Baba Mtakatifu anazo taarifa zote juu ya matokeo ya uchaguzi, kugusia juu y anafasi ya Ujermna iliyo nayo katika ulimwengu kwa namna ya pekee suala la wahamiaji na wakimbizi. Anathibitisha kuwa hili limekuwa suala nyeti ambalo limechukua nafasi kubwa katika mazungumzo yao na katika kubadilishana mawazo.

Aidha Rais Steinmeier anasema, Baba Mtakatifu anaonesha heshima kwa namna ambayo nchi ya Ujermani unawajibika katika kipeo hiki kikubwa cha wahamiaji na kuonesha matumaini ya nchi ya Ujermani akiwatia moyo kwamba wasije geuza mabega katika tatizo hili ambalo bado litazidi kuwapo.
Pamoja na hayo Rais wa Ujermani anasema kuwa, pamoja na wasiwasi mkubwa alio Baba Mtakatifu ni juu ya Bara la Afrika ambapo anawaomba  nchi ya Ujermani iendelee kuchangia kwa juhudi ili kwamba hata mshikamano wa Ulaya uweze kusaidia kuleta maendeleo endelevu kwa nchi ya Afrika mahali ambapo wanatokea wahamiaji wengi sana.

Hata hivyo Baba Mtakatifu pia amekumbuka mabadiliko ya tabia nchi na uhalibifu wa mazingira ambao umesasabisha hata mzunguko huo wa wakimbizi na kuonesha wasiwasi mkubwa ambapo ni matarajio yake kuwa mkataba wa Paris juu ya kipeo hicho unaweza kutkelezwa kikamilifu. Wamezungumzia juu ya nafasi ya Kanisa na dini  na migogoro ya kimataifa. Baba Mtakatifu  anathibitisha mwenyewe kuweza kushiriki kikamilifu pia ni matarajio yake hata makanisa mengine watu wenye mapenzi mema kuweza kuchukulia suala hili kwa moyo mmoja kwa ajili ya ulimwengu uliyo bora .

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 

10/10/2017 09:07