2017-10-09 15:59:00

Upo umuhimu wa kushirikiana katika huduma ya Kanisa na Khalifa wa Petro


Baba Mtakatifu Francisko tarehe 9 Oktoba 2017 amekutana na kuzungumza na Mapatriaki na Maaskofu Wakuu wa Makanisa Katoliki ya Mashariki . Katika hotuba yake anafurahi kuwapokea na kushirikishana furaha na uchungu wa waamini walio kabidhiwa katika shughuli za kichungaji. Anasema, juhudi  hiyo kwa ajili ya Makanisa, inajionesha kwa njia ya umoja na madaraja kuanzia na Askofu wa Roma, ambaye ni Kharifa wa Mtume Petro. Kuwa askofu wa Roma ni msingi wa utume wa Petro ambao ni kwa ajili ya huduma na mkuu wa pendo na katika upendo.

Baba Mtakatifu  anaamini kwamba uhusiano wa Kanisa kati ya ushirika na urithi wa Mtakatifu Petro ni kwa ajili ya  kufanya "urithi msingi wa huduma kama ule wa ushemasi. (Servus Servorum Dei,) ambao unapaswa   kupewa msukumo na thamani katika Kanisa.  Miongoni mwa kazi za mafanikio ya Kharifa  wa mtume  Petro, ni kama vile ya uchaguzi wa Mtume Mattia (Rej : Md1.15-26), upo uhakika wa maaskofu wazuri kwa Makanisa fulani yaliyotawanyika duniani kote. Kwa njia hiyo Baba Mtaktifu anawaomba ushirikiano katika huduma hiyo muhimu , ili kuweza kupata wanaume waaminifu katika huduma hiyo. 

Amemalizia akiwapatia fursa ya kuuliza maswali yao.

 Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.

 








All the contents on this site are copyrighted ©.