2017-10-09 11:46:00

Rais John Pombe Magufuli aliapisha Baraza Jipya la Mawaziri


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli  tarehe 07 Oktoba, 2017 amefanya mabadiliko katika Baraza la Mawaziri kwa kuongeza idadi ya Wizara, kuteua Mawaziri na Naibu Mawaziri wapya na kuwahamisha Wizara baadhi ya Mawaziri na Naibu Mawaziri. Katika mabadiliko hayo Mhe. Rais Magufuli ameongeza idadi ya Wizara na Mawaziri wake kutoka 19 hadi 21, na Naibu Mawaziri kutoka 16 hadi 21.

Iliyokuwa Wizara ya Nishati na Madini imegawanywa na kutakuwa na Wizara ya Nishati na Wizara ya Madini, na iliyokuwa Wizara Kilimo, Mifugo na Uvuvi imegawanywa na kutakuwa na Wizara ya Kilimo na Wizara ya Mifugo na Uvuvi. Rais Magufuli akiwa na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa ametangaza mabadiliko hayo Ikulu Jijini Dar es Salaam na lifuatalo ni Baraza la Mawaziri baada ya kufanyiwa mabadiliko.

Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora. Waziri: George Huruma Mkuchika.

Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).  Waziri:  Selemani Said Jafo Naibu Waziri: Joseph Sinkamba Kandege: Naibu Waziri: George Joseph Kakunda.

Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira: Waziri: January Yusuf Makamba. Naibu Waziri Kangi Alphaxard Lugola.

Ofisi ya Waziri Mkuu: Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu: Waziri Jenista Joackim Mhagama. Naibu Waziri: Anthony Peter Mavunde (Kazi, Vijana na Ajira) Naibu Waziri: Stella Alex Ikupa (Walemavu).

Wizara ya Kilimo. Dkt. Charles John TizebNaibu Waziri: Dkt. Mary Machuche Mwanjelwa.

Wizara ya Mifugo na Uvuvi: Waziri: Luhaga Joelson Mpina. Naibu Waziri: Abdallah Hamis Ulega.

Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano: Waziri: Prof. Makame Mbarawa Mnyaa: Naibu Waziri Mhandisi Atashasta Justus Nditiye pamona na Naibu Waziri: Elias John Kwandikwa.

Wizara ya Fedha na Mipango:  Waziri: Dkt. Philip Isdor Mpango.  Naibu Waziri:Dkt. Ashatu Kijaji.

 Wizara ya Nishati: Waziri: Dkt. Medard Matogoro Kalemani. Naibu Waziri: Subira Hamis Mgalu.

 Wizara ya Madini:  Waziri  Angellah Kairuki. Naibu Waziri: Stanslaus Haroon Nyongo.

 Wizara ya Katiba na Sheria: Waziri: Prof. Palamagamba John Aidan Mwaluko   Kabudi.

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki: Waziri: Dkt. Augustine Philip Mahiga. Naibu Waziri: Dkt. Susan Alphonce Kolimba.

 Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga (JKT): Waziri: Dkt. Hussein Ali Mwinyi

Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi: Waziri: Mwigulu Lameck Nchemba. Naibu Waziri:Mhandisi Hamad Yusuf Masauni.

 Wizara ya Maliasili na Utalii: Waziri: Dkt. Hamisi Andrea Kigwangalla. Naibu Waziri: Josephat Ngailonga Hasunga.

Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi: Waziri: William Vangimembe Lukuvi. Naibu Waziri: Angelina Sylivester Mabula

 Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji: Waziri: Charles Paul Mwijage. Naibu Waziri: Mhandisi Stella Martin Manyanya.

 Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi: Waziri: Prof. Joyce Lazaro Ndalichako. Naibu Waziri: William Tate Ole Nasha.

 Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto:Waziri: Ummy Ally Mwalimu. Naibu Waziri: Dkt. Faustine Engelbert Ndugulile.

 Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo: Waziri: Dkt. Harrison George Mwakyembe. Naibu Waziri: Juliana Daniel Shonza.

 Wizara ya Maji na Umwagiliaji: Waziri: Mhandisi Isack Aloyce Kamwelwe. Naibu Waziri: Jumaa Hamidu Aweso.

Wakati huo huo, Mhe. Rais Magufuli amemteua Bw. Stephen Kagaigai kuwa Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kabla ya Uteuzi huo, Bw. Stephen Kagaigai alikuwa Kaimu Karani wa Baraza la Mawaziri. Bw. Stephen Kagaigai anachukua nafasi ya Dkt. Thomas D. Kashilila ambaye atapangiwa kazi nyingine.

Gerson Msigwa.

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU

Dar es Salaam

07 Oktoba, 2017.








All the contents on this site are copyrighted ©.