2017-10-09 15:31:00

Ni Yesu anaye paka majeraha mafuta na divai na kufunga aliyejeruhiwa


Kuna tabia za kawaida kati yetu za kutazama majanga, mambo mabaya na kuyaacha yalivyo kwa kuangalia na kuangalia upande mwingine. Lakini pia unakuta ni kusoma magazeti ambayo kidogo yamechorwa vituko au mambo mengine yasiyo na maana. Ni maneno ya Baba Mtakatifu Francisko asubuhi ya tarehe 9 Oktoba 2017 wakati wa  mahubiri yake kwenye Kanisa la Mtakatifu Marta mjini Vatican. Baba Mtakatifu anachambua Injili ya siku inayohusu mtu aliye jeruhiwa njiani na majambazi, kwa bahati nzuri akapata mtu wa kumsaidia, lakini ni baada ya kupita wengine wawili wakitazama upande mwingine na kumwacha hapo. 

Baba Mtakatifu anasema huyo alikuwa ni mpagani, mwenye dhambi alikuwa katika safari yake, akaona mtu huyo  lakini hakupita sehemu nyingine au kuangalia upande mwingine, yeye alikuwa ni mwingi wa huruma . Mwinjili Luka anaeleza vizuri historia hiyo, yeye  aliona na akawa na huruma, alimkaribia, hakwenda mbali naye, bali alimkaribia. Alimfunga madonda yake na kumpaka mafuta na divai. Zaidi hakumwacha pale na kuondoka zake.
Katika kutazama hii sehemu, Baba Mtakatiu anaendelea, inakufanya utembue kwa kina ukuu na maajaabu ya Yesu Kristo. Mwalimu wa sheria aliondoka kimya kimya akiwa amejaa aibu, hakutambua. Hakutambua matendo ya Kristo . Labda atakuwa alitambua msingi wa kibinadamu unaotufanya kukaribia ili kutambua  maajabu ya Kristo. Msingi huo ni ule wa kumtazama mwingine kutoka juu hadi chini, hasa anapotaka kumsaidia na umwinua. Hatua hiyo ni moja ya safari njema Baba Mtakatifu anathibitisha,na iwapo anatokea, basi yeye yupo katika safari ya dhati katika kuelekea kwake Yesu.

Kwa nija hiyo Baba Mtakatifu Francisko anatoa maswali kadhaa ya kujiuliza, je mimi ni jambazi, jizi, fisadi, mimi ni kuhani ninaangalia na kutazama upande mwingine? au mimi ni mkatoliki na mwenye madaraka lakini nafanya vilevile? Je mimi ni mdhambi ambaye anapaswa kuhumiwa kwa dhambi zake, lakini ninakaribia, na kumsaidia huyo aliyeumia. Je ninafanya nini mbele ya wenye majaraha, watu wengi ambao ninakutana nao kila siku katika maisha, ninafanya kama Yesu mwenyewe? , ninakuwa mtumishi?
Anamalizia na tafakari ya Injili akiwashauri kurudia kusoma sehemu hiyo kwa makini maana inaonesha maajabu ya Yesu Kristo, Baba Mtakatifu anaongeza kusema,japokuwa hakuwa mdhambi lakini alikuja kwa ajili yetu ili kutuponya na kutoa maisha kwa ajili yetu.

 Sr Angela Rwezaula.
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.