2017-10-09 17:06:00

Bwana atakaporudi atawaondolea ufalme na kuwapa wengine


Yesu aliwaambia wakuu wa makuhani na wazee wa watu, Sikilizeni mfano mwingine. Kulikuwa na mtu mwenye nyumba, naye alipanda shamba la mizabibu akalizungusha ugo, akachimba shimo la shinikizo ndani yake, akajenga mnara, akapangisha wakulima, akasafiri. Wakati wa matunda ulipokuwa karibu, akawatuma watumwa wake kwa wale wakulima, wapokee matunda yake. Wale wakulima wakawakamata watumwa wake, huyu wakampiga na huyu wakamwua, na huyu wakampiga kwa mawe.Akawatuma tena watumwa wengine wengi kuliko wa kwanza, wakawatenda vile vile. Mwishowe akamtuma mwanawe kwao, akisema, Watamstahi mwanangu.

Lakini wale wakulima walipomwona yule mwana wakasemezana wao kwa wao, Huyu ni mrithi; haya na tumwue, tuutwae urithi wake. Wakamkamata, wakamtupa nje ya shamba la mizabibu, wakamwua. Basi atakapokuja yule bwana wa shamba la mizabibu, atawatendaje wale wakulima? Wakamwambia, Atawaangamiza vibaya wale wabaya; na shamba la mizabibu atawapangisha wakulima wengine, watakaomlipa matunda kwa wakati wake.Yesu akawaambia, Hamkupata kusoma katika maandiko, Jiwe walilolikataa waashi, Hilo limekuwa jiwe kuu la pembeni; Neno hili limetoka kwa Bwana, Nalo ni ajabu machoni petu? Kwa sababu hiyo nawaambia, Ufalme wa Mungu utaondolewa kwenu, nao watapewa taifa jingne lenye kuzaa matunda yake.

Mara baada ya kusoma kwa upya Injili ya siku, Baba Mtakatifu anasema hii ni historia inayotugusa maana ni agano ambalo Mungu alifanya na binadamu ambaye anatualika kushiriki. Kama ilivyo kila upendo, hata historia hii inatambuliwa kwa kipindi chake chanya, lakini chenye kuwa na usaliti na kukataliwa. Mwisho wa historia hiyo  wakulima unamalizia na swali, “Je Bwana wa shamba atakaporudi atawanya nini? .Kwa sababu hiyo nawaambia, Ufalme wa Mungu utaondolewa kwenu, nao watapewa taifa jingne lenye kuzaa matunda yake.

Baba Mtakatifu anasisitiza, kukasirika kwa Mungu juu ya tabia na mwenendo wa ubaya wa watu, siyo neno la mwisho! Na hiy ndiyo habari mpya ya Ukristo, Mungu pamoja na kukasirikia udhaifu wetu na dhambi zetu, hakosi neno, wala kusimamia hapo na zaidi kulipiza kisasi. Mungu anapenda, halipizi kisasi, yeye anasubiri ili kusamehe na kutukumbutia. Baba Mtaktifu anasema, Mungu anaendelea kumimina divai mpya ya huruma katika hali ya udhaifu na dhambi, lakini kuna kizingiti kimoja cha utashi mapenzi ya Mungu, nacho ni  masengenyo ambayo kiburi.
Ni mbele ya matendo ya namna hii mahali ambapo hakuna kuzaa matunda, Mungu anakaripia kwa nguvu zake na kuthibitisha,”mtaondolewa ufalme wa Mungu na kupewa watu wanaotoa matunda”.

Kuzaa matunda  ndiyo imani msingi ya maisha ya kikristo, anasema Baba Mtakatifu. Msingi huo siyo wingi wa amri na sheria za kimaadili, bali hawali ya yote ni ushauri wa upendo ambao Mungu kwa njia ya Yesu alifanya na anaendelea kufanya kwa binadamu. Anatoa wito wa kuingia katika historia hii ya upendo , ili kuwa katika shamba la mizabibu lenye uchangamfu, utajiri, wazi, wingi wa matunda na matumaini kwa wote. Hilo liwe shamba amabalo limefunguliwa  kwa kila mazingira, hata kwa wale waliombali zaidi  na wenye shida, maana katika shamba la Bwana alipanda kwa ajili ya wema wa wote anathibitisha Baba Mtakatifu.

Baada ya Sala ya Malaika wa Bwana na kabla ya kuwasalimia mahujaji wote katika Uwaja wa Mtakatifu Petro, Baba Mtatifu anakumbuksa kutangzwa kwa mwenye Jumamosi 7 Oktoba 2017 huko Milano, Padre Arsenio da Trigolo  wa Shirika la ndugu wadogo Wakapuchini ambaye ni mwanzilishi wa Shirika la watawa wa  kike wa Mtakatifu Maria wa Consolata. Anaongeza, ni sifa kwa Mungu kwa ajili ya mnyenyekevu na mtume wake, ambaye pamoja na matendo mengi na majaribu hakuweza kukata tamaa bali daima alikuwa na matumaini. Kwa mujibu wa Kikosi cha walinzi wa Vatican , wanasema walikuwapia wanakaribia waamni 30,00 katuka viwanja vya Mtakatifu Patro kuudhuria sala ya Malaika wa Bwana na Baba Mtaktifu.
Pamoja na hayo taarifa ni kwamba kwa dk tano kulitokea shoti ya spika katika viwaja lakini marekebisho yalifanyika mara na Baba Mtakatifu akaanza upya tena mahubiri yake.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.