Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Kanisa Barani Afrika \ Maendeleo

Sahini ya Jumuiya ya Mt.Egidio na Hospitali ya Mt. Camillo wa ajili ya Afrika

Mkataba usio na malipo wa hospitali ya Mtakatifu Camillo na Jumuiya ya Mt. Egidio, ni habari njema kwa maelfu ya wagonjwa kutoka Afrika na pia Afrika yenyewe - ANSA

07/10/2017 14:14

Umesahiniwa Mkataba tarehe 6 Oktoba 2017 wa ushirikiano katika ya Jumuiya ya Mt.Egidio na Hosptali ya Mt. Camillo-Forlanini mjini Roma. Mkataba huo unatazamia shuguli za mafunzo ya maalumu ya kitaaluma , ikiwa ndani ya Mji wa Roma na baadhi ya nchi za Afrika, lakini pia kusaidia mambo ya kufundisha, kushauri na utafiti. Protokali hizo zimetiwa sahini na Bwana Marco Impagliazzo, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Mtakatifu Egidio  na Fabrizio D’alba Mkurugenzi wa Hospitali ya Mt. Camillo- Forlanini. Prokali  itapanuliwa katika ngazi ya   afya ya mawasiliano, ambayo itawawezesha madakati wa watu wa Roma kutoa huduma bila malipo wakiwa wanatoa huduma hiyo nje ya muda wao wa kuwa katika hospitali, katika kutoa ushauri kwa magonjwa na hasa wale watalaamu wa magonjwa maalumu kama vile ya  moyo, akili na upasuaji.

Mkataba usio na malipo wa hospitali ya Mtakatifu Camillo, ni habari njema kwa maelfu ya wagonjwa kutoka Afrika  ambapo wataweza kwenda kupata ushauri wa kiafya  kwa ngazi ya juu na hata katika hali ngumu ya umasikini au ukosefu wa  zana kwa ajili ya utafiti zaidi wa afya.  Hayo yameelezwa na Bwana Marco Impagliazzo, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Mtakatifu Egidio. Anaongeza kusema kuwa  mpango huo utasaidia kuendeleza mafunzo katika vituo vya afya huko Afrika, mahali ambapo kuna uhaba wa madakita, na hata wataalamu zaidi. Kwa ushirikiano kati ya Jumuiya ya Mtakatifu Egidio na Hospitali ya Mt. Camillo wataweza kukabiliana na matatizo ambayo hadi sasa yamekuwa yakiwekwa pembeni au kutokujali na hasa katika kupambana na magonjwa sugu huko Afrika.

Kwa mujibu wa Taasisi ya utafiti wa juu ya afya inayojishughulisha na magojwa sugu inasema, magonjwa sugu yana tabia mbalimbali na kuonesha dalili zake zinazodumu kwa kipindi na wakati mwingine inaweza kusababisha kupooza kwa mtu. Kwa njia hiyo matibabu yanaweza kuleta unafuu kwa mgonjwa. Na magonjwa sugu yanaweza kujionesha katika hali nyingi, kwa mfano shinikizo, salatani, kisukari, pumu , matatizo ya macho, masikio na magonjwa mengine,yanayoweza kutokana na hali ya hewa au kuambukizwa kama AIDS na epatite. Kwa nchi za Afrika magonjwa hayoyote pia  yanazidi kuongezeka kwa kasi kiasi cha kusababisha vifo vingi kwa miaka 10 ijayo.

Kwa mtazamo wa Hospitali ya Mt. Camillo mpango wa utafiti na ushirikiano wa Kimataifa na Taasisi au Vituo vya afya katika nchi mbalimbali za Afrika ni imara na ya kudumu, kwasababu sasa ni miaka mingi imeweza kutoa madakitari na manesi kila kona ya dunia, anasema Fabrizo Mkurugenzi wa hospitali hiyo. Kwa njia hiyo kutia sahini kwa makataba huo utawezea kuwasaidia kukabiliana na changamoto mpya kwa ushirikiano  na hali halisi na ya aina moja ya Jumuiya ya Mt. Egidio.


Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 

07/10/2017 14:14