Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Baba Mtakatifu Francisko \ Hotuba

Papa Francisko akutana na kuzungumza na Rais wa Croatia

Papa Francisko amekutana na kuzungumza na Rais wa Croatia Bwana Plenkovic

07/10/2017 17:19

Baba Mtakatifu Francisko, Jumamosi tarehe 7 Oktoba 2017 amekutana na kuzungumza na Rais Andrej Plenković wa Jamhuri ya Watu wa Croatia pamoja na ujumbe wake, ambaye baadaye pia amekutana na kuzungumza na Kardinali Pietro Parolin, Katibu mkuu wa Vatican aliyekuwa ameandamana na Monsinyo Antoine Camilleri, Katibu mkuu msaidizi wa mambo ya nchi za nje na ushirikiano wa kimataifa mjini Vatican.

Baba Mtakatifu pamoja na mgeni wake, wamejadili kuhusu uhusiano mwema uliopo kati ya Vatican na Croatia; mchango wa Kanisa katika ustawi, maendeleo na mafao ya familia ya Mungu nchini humo. Wamegusia kuhusu kazi inayoendelea kutekelezwa na Tume ya pamoja ya wataalam kutoka ndani ya Kanisa na Serbia na Croatia kuhusu upembuzi yakinifu mintarafu maisha ya Mwenyeheri Kardinali Alojzije Stepinac. Baadaye, wamejielekeza zaidi katika masuala ya kikanda na kimataifa, hasa zaidi kuhusu hatima ya Umoja wa Ulaya kwa siku za usoni hasa zaidi kuhusiana na maisha ya wananchi wa Croatia, Bosnia na Erzegovina.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.

07/10/2017 17:19