Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Kanisa Barani Afrika \ Amani

MALI: Wasiwasi wa Maaskofu kutokana na mashambulizi ya Makanisa yao

tukio moja kubwa lilitokea wiki iliyopita huko Dobora kilimita 800 kutoka mji Mkuu Bamako,na kwamba makundi yenye silaha walibomoa kwa nguvu milango ya Makanisa na kuchoma moto misalaba, - AFP

06/10/2017 09:04

Maaskofu nchini Mali wanawasiwasi baadaya ya mashambulizi ya Makanisa, na vikanisa vidogo katikati ya  nchi, mahali  ambapo wakatoliki ni asilimia 2% ya watu wote kutokana na kwamba sehemu kubwa ya watu ni waislamu.  “Katika siku za hivi karibuni , makanisa yetu na vikanisa vidogo, vimekuwa ndiyo uwanja wa mashabulizi ya majeshi ya kijihadi, hivyo wasiwasi mkubwa tulio nao”. Ni maneno yaliyotamkwa kwenye Shirika la habari la France na katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Padre Edmond Dembélé. Anasema, tukio moja kubwa lilitokea wiki iliyopita huko Dobora kilomita 800 kutoka mji Mkuu  Bamako,na kwamba makundi yenye silaha walibomoa kwa nguvu milango ya Makanisa na kuchoma moto misalaba, picha mbalimbali zikiwemo sanamu za Mama Maria na vitambaa vya altareni. Padre Ndebele, anaendelea, mashambulizi mengine ya Makanisa na vikanisa vidogo yametokea hata mbele ya waamini wiki chache za nyuma. Katika maeneo ya Bodwal, katikati ya mji, watu walifukuzwa ndani ya makanisa na vikundi vyenye silaha, wakiwatishia kuwauwa iwapo watawakuta tena ndani ya majengo hayo.

Hali ya kisiasa nchini mali siyo nzuri kutokana na makundi ya  Wanamgambo wa Kiislamu wa Ansar Dine na washirika wao kutumia  fursa ya uasi uliyofanywa na Watuareg kaskazini mwa Mali, machi 2012, ambapo. Hao wanathibiti karibu mbili ya tatu ya eneo la jangwa, lililo na miji ya kihistoria ya Gao, Kidal na Timbuktu, ambako turaathi muhimu za dini ya kiislam ziliharibiwa wakati wa mapambano. Hata hivyo baadaya   wanajeshi wa kimataifa kuongozwa na  Ufaransa na 2013 waliwezesha kuwafukuza makundi hayo katika sekemu kubwa, lakini wengine wamekimbilia katika maeneo ambayo hayaeleweki na nguvu za vikosi vya kimataifa vya kulinda amani.Taarifa zinasema, pamoja na kusaini mkataba 2015 wa amni na kundi hilo, bad hali inaendela kujitokeza.

Hali ya ukosefu wa usalama kwa upya katika miaka ya hii ya nwisho inaendelea kuwa mbaya kutoshia  maisha ya watu wa Mali, hasa kwa sehemu katikati ya  Mali, ambapo bado kuna makundi ya kutumia silaha ya kiislaam. Kwa mujibu wa ripoti za hivi karibuni za Mashirika ya kibinabadanu , wanathibitisha kuwa, makundi  haya ni hatari katika kishambuliwa taifa la Mali, kwa maana wanaharibu shule na kuwateka watoto ambao baadaye wanafundishwa kudhika silaha.

Sr Angela Rwezaula

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 

06/10/2017 09:04