Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Baba Mtakatifu Francisko \ Katekesi siku ya Jumatano

Papa Francisko: utangulizi wa Sinodi ya vijana: 19-24 Machi 2018

Papa Francisko asema, kuanzia tarehe 19-24 Machi 2018 kutakuwa na utangulizi wa maadhimisho ya Sinodi ya Maaskofu kwa ajili ya vijana.

04/10/2017 13:56

Baba Mtakatifu Francisko mara baada ya Katekesi yake juu ya matumaini ya Kikristo, Jumatano, tarehe 4 Oktoba 2017 ametangaza kwamba kuanzia tarehe 19 Marchi 2018 Sherehe ya Mtakatifu Yosefu mchumba wake Bikira Maria hadi tarehe 24 Machi 2018, kutaadhimishwa utangulizi wa Sinodi ya Maaskofu kwa ajili ya vijana inayoongozwa na kauli mbiu “Vijana, Imani na Mang’amuzi ya Miito”.

Baba Mtakatifu anasema, hii ni safari ya maisha ya Kanisa katika kujenga utamaduni wa kuwasikiliza vijana, kuwajali, kuimarisha imani pamoja na kusikiliza changamoto zinazotolewa na vijana wa kizazi kipya. Hitimisho la maadhimisho haya litawasilishwa kwa Mababa wa Sinodi ya Maaskofu itakayoadhimishwa rasmi mwezi Oktoba, 2018.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.

04/10/2017 13:56