Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Kanisa \ Kanisa Ulimwenguni

Yerusalem:Jumuiya mpya ya ndugu wadogo wa Mt.Francis wa Asizi

Jumuiya mpya wa familia za kifranciskani kufunguliwa katika madhabahu ya Emmau Yerusalem, hao ni Waoservanti na Wakonventuali - ANSA

03/10/2017 15:40

Kwa mujibu wa maandishi Matakatifu ya Injili , mitume wa Emmau hawakuwa na utambuzi wa ufufuko wa Yesu, lakini Bwana akawaongoza katika safari yao na kuwapa matumaini na uwezo wa kumtambua wakati wa kuumega mkate. Hiyo ni hatua ambayo pia inaweza kujitokeza katika maisha wa wengi, iwapo hawamkaribishi Yesu aweze kukaa nao daima kama walivyotenda wale  wafuasi wa Yesu huko Emmau. 

Ni maneno ya Padre Francisko Patton, msimamizi wa maeneo Matakatifu Yerusalemu wakati wa mahubiri yake kwanye misa ya uzinduzi wa Jumuiya mpya ya ndugu wadogo wa Mtakatifu Francisko wa Asizi kwenye Madhabahu ya Emmau mapema wiki hii. Misa hiyo imekwenda sambamba na kukumbukumbu ya mitume wa Yesu Simioni na Cleopa kilomita chache kutoka Mji wa Yerusalemu. Uzinduzi wa Jumuiya mpya unaundwa na familia mbili za kifransiscani yaani wafrasiskani wadogo wa Waoservanti na Wakonventuali ambapo Padre Patton  anasema ina maana kubwa kwa mwaka 2017 kutokana na kukumbuka maadhimiso ya miaka 500 tangu uwepo wa wafranciskani katika maeneo ya Emma una tukio moja muhimu katika maisha ya familia ya kifransiskani.

Padre Patton anasema tukio la kuzinduliwa Jumuiya mpya ya ndugu wadogo ni katika kuendeleza kutoa huduma ya kukaribisha mahujaji katika madhabahu hiyo, na kutoa fursa ya wale wote wanao taka kusali, kutafakari na kujifunza. Aidha  Padre Pattoni anasema hii ni kuendeleza kutoa ushuhuda wa muungano na ushirikiano wa kindugu mara baada ya majaribio ya mgawanyiko uliotokea  mwaka 1517  na kusababisha uchungu mkubwa wa Shirika la kifransiskani. Kwa namna hiyo hii itakuwa ni neema kwa ndugu wadogo ambao watakuwapo wanaishi roho ya mahali pale na watajisikia ile tasaufi ya mitume wa Emmau.

Na kwa mujibu wa Mkuu wa Shirika la ndugu wadogo wa Wakonvetuali, padre Jerzy Norel anasema, Jumuiya ya Emmau imaeanzishwa kwa ajili ya umoja wa kifransikani ambao unajikita katika kushi kwa umoja na kukakaribisha wengine ili waweze kuishi katika umoja. Hata Mkuu wa Shirika la ndugu wadogo wa Waoservanti, Padre Julio César Bunader amethibitisha  kuwa, kuundwa kwa jumuiya mpya katika mtazamo wa maadhimisho ya miaka 500 ya uwepo katika maeneo hayo ni kutaka kufanya hatua katika ngazi ya maisha, kindugu na utume. Na kwa njia hiyo ni kuthibitisha maneno ya Mtakatifu Francisko wa Asizi kuwa “kila ndugu ni zawadi kwa Bwana. Kwa njia hiyo ndugu wadogo watakao kwenda kuishi katika Konventi hiyo ni zawadi.

Ikumbukwe mnamo mwaka 1517 ulizuka utengano wa Waoservanti na Wakonventuali kati yao pamoja na kwamba ni shirika moja wa ndugu wadogo wa Mtakatifu Francisko wa Asizi.

Sr Angela Rwezaula 
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 

03/10/2017 15:40