2017-10-03 15:30:00

Kard. Sandri amehitimisha ziara yake ya kitume nchini Romania


Tarehe 1 Oktoba, Kardinali Sandri Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa kwa ajili  Makanisa ya Mashariki amehitimisha ziara yake  nchini Romania. Jumapili asubuhi aliondoka asubuhi na mapema kutoka Makao Makuu ya Kiasikofu ya  Kigiriki Katoliki kuelekea karibu na Makao Makuu ya Kardinali Lucien Muresan, akiwa amesindikizwa na Balozi wa Vatican nchini   Romania, Askofu Mkuu Maury Buendia. Mara baada ya kifungua kinywa akiwa na  na  Sinodi nzima ya Maskofu na mapadre wamejianda katika Liturujia ya Kipapa iliyo anza majira ya  saa nne asubuhi kwenye Kanisa Kuu la Romani. Misa iliudhuriwa mapadre  zaidi ya mia moja na waamini wengi wa Romania.

Kabla ya kuanza misa na baada ya misa, Kardinali Muresan alitoa hotuba fupi ya makaribisha  pia kumtakia mema Kardinali Sandri, ikiwa ni pamoja na Baraza lake  la Kipapa kwa ajili ya Makanisa ya Mashariki, maadhimisho ya miaka 50 ya kupata padre wa kwanza katika nchi hiyo, na zaidi pia kumuomba Kardinali kwa dhati afikishe  salam kwa Baba Mtakatifu kutoka kwa waamini wote wa Romania wanao msindikiza katika sala na ili siku moja iweze kutimiza ndoto yao ya Baba Mtakatifu kutembelea Taifa la  Romania.

Naye Kardinali Sandri katika mahubiri yake anasema,kutoa sadaka katika maisha ndiyo njia mwalimu na  kuwa waaminifu wa leo katika kurithi imani iliyooneshwa  na mababa na walimu wa imani, japokuwa haitoshi tu kutazama ushahidi wao au  kuufanya utambulike na wengine kwa shangwe kuu; hiyo ni lazima wao wawe mfano wa kuigwa na uwe mwamko wa kufuata nyayo zao na zile za Kristo.

Kardinali Sandri anayasema hayo akikumbuka wafia dini na  waathirika walioteswa na kuwawa wakati utawala wa udikiteta nchini Romania. Na kwa njia hiyo anakumbuka hati ambayo iko kwenye mchakato wa kuwatangaza wenye heri na watakatifu kwa baadhi ya waamini waliotoa maisha yao kama sadaka ya kuteketezwa. Hao ni pamoja na maaskofu walitoa toa maisha yao kwenye magereza ya utawala wa kidikteta huko Romania. Anawaomba wazidi kusali kwa matumaini ili majina yao yaweze kuandikwa katika kitabu cha wenye heri na watakatifu. Anawashukuru wote wanaojikita katika  mchakato wa utambuzi na kwamba wazidi kuomba kwani sala ni  mchango mkubwa wa kufikia siku hiyo ya kutengzwa kwao.

Akitafakari juu ya Injili anasema, Yesu anatoa mwito  wa kuwa na tabia ya kiamaadili ya Mungu  anavyotoa huruma yake kwetu sisi kila siku; hata huruma ya Liturujia ambayo wanaadhimisha, Kardinalia anasema, ni kama mlango wazi ambao unawaruhusu kutembea hadi kuufikia ile sadaka ya kujitoa kama Yesu alivyojitoa msalabani  kwa ajili ya wote, lakini  Baba yake amkarudishia maisha hayo siku ya Pasaka. Iwapo  hawatambui neema hiyo kama Yesu anavyotaka kwa kila mmoja,  imani yao inabaki ya kijujuu tu ambayo haigusi roho.

Bwana Yesu anataka watu wake wapambane dhidi ya ubaya unaozidi kutambaa katika ulimwengu kwa njia mbalimbali, na  tofauti za nguvu ya ubaya huo , na kwa namana hiyo ni kutafakari kwa upya Injili hasa kwa kutafakari Yeye mwenyewe msulibiwa. Kardinali anaongeza , dunia haiwezi kubadilika au kutawala kwa mipango au mapendekezo yenye matashi mema ya watu wake tu, hiyo ni kwasababu  imekwisha kombolewa na Kristo. Ni lazima kujikabidhi kila siku katika ile “NDIYO” ya  Bwana wetu  Yesu Kristo aliyotamka.

Kabla ya Baraka ya mwisho Kardinali Sandri wametoa zawadi kwa Askofu Mkuu Muresan, Medali ya shaba inayokumbusha mwaka wa tano  wa utume wa Upapa wa Baba Mtakatifu Francisko. Medali hiyo ni ishara pia ya kutoa wito wa mada nyeti ya sasa juu ya makaribisho ya wahamiaji, wakimbizi na hasa  hali halisi  watu milioni kati  nne na sita ya waromania walioko katika bara la Ulaya na duniani, walioondoka katika nchi yao kwa miaka mingi ili kutafuta kazi na maisha bora.

Pamjia na misa hiyo ni ishara na muhuri ambao ahutatoka  katika mioyo ya nchi  Romania kwababu ya maandamano ya maaskofu, mapadre na  waamini wote kuelekea katika mtaa wa Kabila la Waromania ili kubariki jiwe la msingi kwa ajili ya ujenzi wa Kanisa la kichungaji kwa mujibu wa ratiba yao iliyo kuwa imepangwa. Katika tukio hilo, shangwe, vigelele na nyimbo zilizotumbuizwa na watoto na vijana kutoka  kituo cha watoto yatima vilevile kutoka kwa watu wa mitaa hiyo wakisindikizwa na  maapadre na watawa wanao wasindikiza katika shughuli za kichungaji nchini Romania.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.