2017-10-02 11:49:00

Papa :tokeni nje ya viota vya ubinafsi ili kuhudumia maskini wa Mungu


Baba Mtakatifu mara baada ya hotuba yake katika uwanja wa Cesena, amekwenda moja kwa moja katika kanisa Kuu la Cesena , mahali ambapo amepokelewa na watoto na vijana.  Baada ya kuingia Kanisa Kuu imefuatiwa hotuba fupi ya Askofu Douglas Regattieri, wa  Cesena-Sarsina.Naye Baba Mtakatifu katika hotuba yake, anawashukuru wote kwa ukarimu wao katika ziara hiyo. Amewaonesha ukaribu wake katika shughuli zao za kichungaji za kupeleka mbele ushuhuda wa uinjilishiji. Anasema huo ndiyo utume na msingi kwa wafuasi wa Kristo kutangaza na kushuhudia furaha ya Injili. 

Baba Mtakatifu anafafanua juu ya kuinjilisha kuwa ni hatua madhubuti ambayo ni lazima kuifanya kwa umakini na kwa mshikamano wa dhati katika hali halisi ya Kanisa na watu wake , wakati huo huo wakiwa na kitovu cha kufikia kwa usalamayaani uwepo wa Askofu wa jimbo kama kiongozi wao mkuu katika shughuli zote za kichungaji jimbo. Baba Mtakatifu anaelezea juu ya  maana ya uwajibikaji kwamba ni neno au ufunguo wa kupeleka kazi ya utume mbele katika makambi ya katekesi, elimu Katoliki na kuhamasisha maisha ya binadamu kwa upendo.Anawataka waondoke katika kiota cha ubinafsi na kutoa kwa ujasiri katika jumuiya nzima.

Vilevile anabaishainisha kuwa inahitaji ujasiri mkubwa mbele ya changamoto za kichungaji na kijamii pia katika aina mpya za mshikamano zilizopo katika Kanisa mahalia.Anasisitiza juu ya ushirikiano na kuhepukana na mivitano , uchochezi na masengenyo, ambapo maerudia kusema kuwa anayefanya masengenyo ni gaidi. Kwa maana anatupa bomu na kuondoka,bomu hilo linahumiza wengi. Ni lazima kuhepuka masengenyo ndani ya jumuiya za kitawa, parokia, mapadre na katika vyama na makundi ya kichungaji katika jimbo!

Kanisa mahali ni ushuhuda tayari wa imani kwa maana ya kuona Kanisa katika kujikita kwa undani kutembea kindugu na umoja anasema Baba Mtakatifu na kusisitiza kuwa bila mshakamano, ushuhuda na imani mambo mengine hayana faida.
Kuna majeraha ya Kristo yanayobaki wazi na kuoneka kwa wote hasa wanao ishi pembezoni mwa jamii na umaskini. Ni watu ambao wamejeruhiwa katika majaribi mengi ya maisha ndiyo hapo Kanisa linahitaji kwenda kupeleka harufu ya mchungaji mwema. Anasisitiza ni umoja pia uwezo wa kuondokana na ubinafsi ili kuweza kutoa huduma bila kijibakiza, ndiyo utume ambao Yesu mwenyewe anaagiza kwenda kukutanana ndugu walio jeruhiwa, wenye mahitaji, walio baguliwa na jamii, walio na upweke. 

Baba Mtakatifu akiwageukia Mapadre na watawa na walei  wote wanaoojikita katika utume kichungaji  anawaeleza kuwa ni lazima kuwa na uhusiano karibu na Bwana kwa njia ya sala na tafakari, sala ambazo zinawaimarisha katika ukuhani wao na utume wao kwa wote ili kuweza  kupata nguvu ya kwenda katika utume waliokabidhiwa. Hawali ya yote  waoneshe furaha katika kuinjilisha na katika utume kwa watu kwa maana wamakebidhiwa kundoo wao.

 Akisisitiza juu ya kwenda nje , amewakumbusha juu kuwa na uwezeo wa kutazama upeo wa juu zaidi mtazamo wa Yesu , ili kkuweza kukabiliana na mapinduzi ya sasa, lakini mapinduzi ya ukarimu na wrma ambayo inawasaifia kujua namna ya kutoa mang’amuzi.Na hiyo pia ni katika mzatazamo wa vijana ambao Baba Mtakatifu anasema ndiyo tegemo la Kanisa. Ni lazima kukutana nao, kuwasikiliza, kutembea nao ili nao waweze kukutana na Kristo na ujumbe wake wa upendo unao toa uhuru kutokana na minyororo ya kiulimwengu. Baba Mtakatifu ya hotuba yake amekutana na kuzungumza kidogo na wageni wa nyumba ya mapokezi ya jimbo na watu wa kujitolea walio andaa ziara yake jimboni. Baadaye aliondoka na gari hadi kiwanja cha ndegu na kuwaaga viongozi walio mpokea saa  nane asubuhi kuelekea Bologna.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.