2017-10-02 15:52:00

Papa: Inawezakena kushirikishana ili kukabiliana na kipeo cha ajira


Baba Mtakatifu Francisko akihutubia kwa ulimwengu wa wafanyakazi mjini Bologna, Jumapili tarehe 1 Oktoba 2017 anaonesha wasiwasi wa hali halisi ya kipeo cha fursa za ajira, ambapo anasema kwa bahati  mbaya ipo hali ngumu inayosababibishwa na ukosefu wa ajira katika jamii. Akiwaelekeza wote, anasema, wao wanawakilisha jamii mbalimbali zenye kuishi kwa uchungu, lakini wakati huo huo wanajifunza kuwa kwa pamoja ni rahisi kuondokana na kipeo hicho katika ujenzi wa maisha endelevu.  Baba Mtakatifu anabainisha kuwa, hali hiyo inawezekana kwa njia ya mazungumzo ya pamoja, katika kutafuta majibu mazuri na muhimu  ya ubunifu kwa kila mtu, lakini ikiwa ni pamoja na ubora wa kazi, hasa ustawi wa lazima katika maisha yabinadamu anaongeza: hiyo ndiyo wengine wanaiita mfumo wa Emilia. Baba Mtakatifu anawahimiza wajikite zaidi katika kupeleka mbele kwa maana kuna haja ya kutafuta ufumbuzi thabiti na uwezo wa kusaidia katika kutazama hali halisi endelevu ili kukidhi haja ya mahitaji ya watu na familia.

Anaendelea na hotuba yake kuwa, katika wilaya yao upo uzoefu wa ushirika ambao umedumu kwa muda mrefu, na kwamba umetokana na thamani ya msingi ya ushirikiano. Leo hii bado kuna mengi ya kutoa, hata kusaidia wengi ambao wana shida na wanahitaji  yaani  kuwapa "lift ya kijamii" ambayo kwa mujibu wa baadhi ya wengine haina na matumizi Baba Mtakatifu anabainisha. Mshikamano kamwe hauna mshahara,  wala ile mantiki ya faida ya kifedha ambayo ingekuwa na  sababu ya kuindoa. Kwa maneno hayo Baba mtakatifu anaongeza na mara nyingine hiyo inaibiwa kwa kwa wale wadhaifu ambao wanahitaji. Kwa njia hiyo, anasisitiza kuwa, wajaribu kutafuta jamii ya haki zaidi na isiwe ndoto ya kizamani, bali katika kujikita kwa bidii kwenye kazi ambayo kila mtu leo hii anahitaji.

Baba Mtakatifu anawafikiria vijana wengi na wale wengine  ambao wamepoteza kazi , au hawezi kupata fursa hiyo. Lakini pia anawashauri kuwa kukaribisha na kupambana na umaskini kwa upande mkubwa unapitia kwa njia ya  kazi . Siyo rahisi  kutoa msaada wa kweli kwa maskini iwapo hauna kazi na hadhi. Hiyo ni changamoto kubwa katika miaka hii ya ujenzi mpya baada ya vita vilivyo acha umaskini kupindukia.
Kwa njia hiyo Baba Mtakatifu  amekumbuka Mkataba wa kazi unaotazama sehemu zote za kijamii, hata Kanisa. Mkataba ulio tiwa saini unajikita kwa wote kusaidia kutafuta majibu endelevu na kwamba siyo kama sadaka lakini ni mtindo muhimu ambao yeye mwenyewe binafsi anasema kuwa na matumaini ya kuzaa matunda yanayotarajiwa.

Kipeo cha uchumi kinaikumba Ulaya na Ulimwengu mzima, Baba Mtakatifu anasema, lakini kama itambulikanavyo pia kipeo hicho kinahusu maadili, kiroho na kibinadamu. Hiyo yote inatokana na mzizi wa usaliti wa faida ya watu binafsi hata katika makundi ya kiutawala anasema Baba Mtakatifu. Hawa wanatumia masalhai binafsi badala ya wote katika jamii kwa njia hiyo, Baba Mtakatifu Francisko anasisitiza, kuwa kuna ulazima wa kuongeza fursa za kazi yenye kuleta hadhi. Hiyo ndiyo wajibu mkubwa inaohusu jamii nzima, kwa namna ya pekee vyombo vya utawala kijamii na mambo yake yote. Aidha  wote wanaalikwa kufanya juhudi zote ili kazi ambayo ni msingi wa binadamu kwa wote ipewe kipaumbele zaidi.

Sr Angela Rwezaula 
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.